# ar/Arabic.xml.gz
# ss/Swahili-NT.xml.gz


(src)="b.MAT.1.1.1"> كتاب ميلاد يسوع المسيح ابن داود ابن ابراهيم .
(trg)="b.MAT.1.1.1"> Yesu Kristo alikuwa mzawa wa Daudi , mzawa wa Abrahamu .
(trg)="b.MAT.1.1.2"> Hii ndiyo orodha ya ukoo wake :

(src)="b.MAT.1.2.1"> ابراهيم ولد اسحق . واسحق ولد يعقوب . ويعقوب ولد يهوذا واخوته .
(trg)="b.MAT.1.2.1"> Abrahamu alimzaa Isaka , Isaka alimzaa Yakobo , Yakobo alimzaa Yuda na ndugu zake ,

(src)="b.MAT.1.3.1"> ويهوذا ولد فارص وزارح من ثامار . وفارص ولد حصرون . وحصرون ولد ارام .
(trg)="b.MAT.1.3.1"> Yuda alimzaa Faresi na Zera ( mama yao alikuwa Tamari ) , Faresi alimzaa Hesroni , Hesroni alimzaa Rami ,

(src)="b.MAT.1.4.1"> وارام ولد عميناداب . وعميناداب ولد نحشون . ونحشون ولد سلمون .
(trg)="b.MAT.1.4.1"> Rami alimzaa Aminadabu , Aminadabu alimzaa Nashoni , Nashoni alimzaa Salmoni ,

(src)="b.MAT.1.5.1"> وسلمون ولد بوعز من راحاب . وبوعز ولد عوبيد من راعوث . وعوبيد ولد يسى .
(trg)="b.MAT.1.5.1"> Salmoni alimzaa Boazi ( mama yake Boazi alikuwa Rahabu ) .
(trg)="b.MAT.1.5.2"> Boazi na Ruthi walikuwa wazazi wa Obedi , Obedi alimzaa Yese ,

(src)="b.MAT.1.6.1"> ويسى ولد داود الملك . وداود الملك ولد سليمان من التي لأوريا .
(trg)="b.MAT.1.6.1"> naye Yese alimzaa Mfalme Daudi .
(trg)="b.MAT.1.6.2"> Daudi alimzaa Solomoni ( mama yake Solomoni alikuwa mke wa Uria ) .

(src)="b.MAT.1.7.1"> وسليمان ولد رحبعام . ورحبعام ولد ابيا . وابيا ولد آسا .
(trg)="b.MAT.1.7.1"> Solomoni alimzaa Rehoboamu , Rehoboamu alimzaa Abiya , Abiya alimzaa Asa ,

(src)="b.MAT.1.8.1"> وآسا ولد يهوشافاط . ويهوشافاط ولد يورام . ويورام ولد عزيا .
(trg)="b.MAT.1.8.1"> Asa alimzaa Yehoshafati , Yehoshafati alimzaa Yoramu , Yoramu alimzaa Uzia ,

(src)="b.MAT.1.9.1"> وعزيا ولد يوثام . ويوثام ولد آحاز . وآحاز ولد حزقيا .
(trg)="b.MAT.1.9.1"> Uzia alimzaa Yothamu , Yothamu alimzaa Ahazi , Ahazi alimzaa Hezekia ,

(src)="b.MAT.1.10.1"> وحزقيا ولد منسّى . ومنسّى ولد آمون . وآمون ولد يوشيا .
(trg)="b.MAT.1.10.1"> Hezekia alimzaa Manase , Manase alimzaa Amoni , Amoni alimzaa Yosia ,

(src)="b.MAT.1.11.1"> ويوشيا ولد يكنيا واخوته عند سبي بابل .
(trg)="b.MAT.1.11.1"> Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake .
(trg)="b.MAT.1.11.2"> Huo ulikuwa wakati Wayahudi walipopelekwa uhamishoni Babuloni .

(src)="b.MAT.1.12.1"> وبعد سبي بابل يكنيا ولد شألتيئيل . وشألتيئيل ولد زربابل .
(trg)="b.MAT.1.12.1"> Baada ya Wayahudi kupelekwa uhamishomi Babuloni : Yekonia alimzaa Shealtieli , Shealtieli alimzaa Zerobabeli ,

(src)="b.MAT.1.13.1"> وزربابل ولد ابيهود . وابيهود ولد الياقيم . والياقيم ولد عازور .
(trg)="b.MAT.1.13.1"> Zerobabeli alimzaa Abiudi , Abiudi alimzaa Eliakimu , Eliakimu alimzaa Azori ,

(src)="b.MAT.1.14.1"> وعازور ولد صادوق . وصادوق ولد اخيم . واخيم ولد اليود .
(trg)="b.MAT.1.14.1"> Azori alimzaa Zadoki , Zadoki alimzaa Akimu , Akimu alimzaa Eliudi ,

(src)="b.MAT.1.15.1"> واليود ولد أليعازر . وأليعازر ولد متان . ومتان ولد يعقوب .
(trg)="b.MAT.1.15.1"> Eliudi alimzaa Eleazeri , Eleazeri alimzaa Mathani , Mathani alimzaa Yakobo ,

(src)="b.MAT.1.16.1"> ويعقوب ولد يوسف رجل مريم التي ولد منها يسوع الذي يدعى المسيح .
(trg)="b.MAT.1.16.1"> Yakobo alimzaa Yosefu , aliyekuwa mume wake Maria , mama yake Yesu , aitwaye Kristo .

(src)="b.MAT.1.17.1"> فجميع الاجيال من ابراهيم الى داود اربعة عشر جيلا . ومن داود الى سبي بابل اربعة عشر جيلا . ومن سبي بابل الى المسيح اربعة عشر جيلا
(trg)="b.MAT.1.17.1"> Basi , kulikuwa na vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka Daudi , vizazi kumi na vinne tangu Daudi mpaka Wayahudi walipochukuliwa mateka Babuloni , na vizazi kumi na vinne tangu kuchukuliwa mateka mpaka wakati wa Kristo .

(src)="b.MAT.1.18.1"> اما ولادة يسوع المسيح فكانت هكذا . لما كانت مريم امه مخطوبة ليوسف قبل ان يجتمعا وجدت حبلى من الروح القدس .
(trg)="b.MAT.1.18.1"> Basi , hivi ndivyo Yesu Kristo alivyozaliwa : Maria , mama yake , alikuwa ameposwa na Yosefu .
(trg)="b.MAT.1.18.2"> Lakini kabla hawajakaa pamoja kama mume na mke , alionekana kuwa mja mzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu .

(src)="b.MAT.1.19.1"> فيوسف رجلها اذ كان بارا ولم يشأ ان يشهرها اراد تخليتها سرّا .
(trg)="b.MAT.1.19.1"> Yosefu , mumewe , kwa vile alikuwa mwadilifu , hakutaka kumwaibisha hadharani ; hivyo alikusudia kumwacha kwa siri .

(src)="b.MAT.1.20.1"> ولكن فيما هو متفكر في هذه الامور اذا ملاك الرب قد ظهر له في حلم قائلا يا يوسف ابن داود لا تخف ان تأخذ مريم امرأتك . لان الذي حبل به فيها هو من الروح القدس .
(trg)="b.MAT.1.20.1"> Alipokuwa bado anawaza jambo hilo , malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto , akamwambia , " Yosefu , mwana wa Daudi , usiogope kumchukua Maria awe mke wako , maana amekuwa mja mzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu .

(src)="b.MAT.1.21.1"> فستلد ابنا وتدعو اسمه يسوع لانه يخلّص شعبه من خطاياهم .
(trg)="b.MAT.1.21.1"> Atajifungua mtoto wa kiume , nawe utampa jina Yesu , kwa kuwa yeye atawaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao . "

(src)="b.MAT.1.22.1"> وهذا كله كان لكي يتم ما قيل من الرب بالنبي القائل .
(trg)="b.MAT.1.22.1"> Basi , haya yote yalitukia ili litimie lile neno Bwana alilosema kwa njia ya nabii :

(src)="b.MAT.1.23.1"> هوذا العذراء تحبل وتلد ابنا ويدعون اسمه عمانوئيل الذي تفسيره الله معنا
(trg)="b.MAT.1.23.1"> " Bikira atachukua mimba , atamzaa mtoto wa kiume , naye ataitwa Emanueli " ( maana yake , " Mungu yu pamoja nasi " ) .

(src)="b.MAT.1.24.1"> فلما استيقظ يوسف من النوم فعل كما امره ملاك الرب واخذ امرأته .
(trg)="b.MAT.1.24.1"> Hivyo , Yosefu alipoamka usingizini alifanya kama malaika huyo alivyomwambia , akamchukua mke wake nyumbani .

(src)="b.MAT.1.25.1"> ولم يعرفها حتى ولدت ابنها البكر . ودعا اسمه يسوع
(trg)="b.MAT.1.25.1"> Lakini hakumjua kamwe kimwili hata Maria alipojifungua mtoto wa kiume .
(trg)="b.MAT.1.25.2"> Naye Yosefu akampa jina Yesu .

(src)="b.MAT.2.1.1"> ولما ولد يسوع في بيت لحم اليهودية في ايام هيرودس الملك اذا مجوس من المشرق قد جاءوا الى اورشليم
(trg)="b.MAT.2.1.1"> Yesu alizaliwa mjini Bethlehemu , mkoani Yudea , wakati Herode alipokuwa mfalme .
(trg)="b.MAT.2.1.2"> Punde tu baada ya kuzaliwa kwake , wataalamu wa nyota kutoka mashariki walifika Yerusalemu ,

(src)="b.MAT.2.2.1"> قائلين اين هو المولود ملك اليهود . فاننا رأينا نجمه في المشرق واتينا لنسجد له .
(trg)="b.MAT.2.2.1"> wakauliza , " Yuko wapi mtoto , Mfalme wa Wayahudi , aliyezaliwa ?
(trg)="b.MAT.2.2.2"> Tumeiona nyota yake ilipotokea mashariki , tukaja kumwabudu . "

(src)="b.MAT.2.3.1"> فلما سمع هيرودس الملك اضطرب وجميع اورشليم معه .
(trg)="b.MAT.2.3.1"> Mfalme Herode aliposikia hayo , alifadhaika , yeye pamoja na wakazi wote wa Yerusalemu .

(src)="b.MAT.2.4.1"> فجمع كل رؤساء الكهنة وكتبة الشعب وسألهم اين يولد المسيح .
(trg)="b.MAT.2.4.1"> Basi akawaita pamoja makuhani wakuu wote na walimu wa Sheria , akawauliza , " Kristo atazaliwa wapi ? "

(src)="b.MAT.2.5.1"> فقالوا له في بيت لحم اليهودية . لانه هكذا مكتوب بالنبي .
(trg)="b.MAT.2.5.1"> Nao wakamjibu , " Mjini Bethlehemu , mkoani Yudea .
(trg)="b.MAT.2.5.2"> Ndivyo nabii alivyoandika :

(src)="b.MAT.2.6.1"> وانت يا بيت لحم ارض يهوذا لست الصغرى بين رؤساء يهوذا . لان منك يخرج مدبر يرعى شعبي اسرائيل
(trg)="b.MAT.2.6.1"> Ewe Bethlehemu katika nchi ya Yuda , kwa vyovyote wewe si mdogo kabisa kati ya viongozi wa Yuda ; maana kwako atatokea kiongozi atakayewaongoza watu wangu , Israeli . "

(src)="b.MAT.2.7.1"> حينئذ دعا هيرودس المجوس سرّا وتحقق منهم زمان النجم الذي ظهر .
(trg)="b.MAT.2.7.1"> Hapo , Herode aliwaita faraghani hao wataalamu wa nyota , akawauliza wakati hasa ile nyota ilipowatokea .

(src)="b.MAT.2.8.1"> ثم ارسلهم الى بيت لحم وقال اذهبوا وافحصوا بالتدقيق عن الصبي . ومتى وجدتموه فاخبروني لكي آتي انا ايضا واسجد له .
(trg)="b.MAT.2.8.1"> Kisha akawatuma Bethlehemu akisema , " Nendeni mkachunguze kwa makini habari za mtoto huyo .
(trg)="b.MAT.2.8.2"> Mkisha mpata nileteeni habari ili nami niende nikamwabudu . "

(src)="b.MAT.2.9.1"> فلما سمعوا من الملك ذهبوا واذا النجم الذي رأوه في المشرق يتقدمهم حتى جاء ووقف فوق حيث كان الصبي .
(trg)="b.MAT.2.9.1"> Baada ya kumsikiliza mfalme , hao wataalamu wa nyota wakaenda .
(trg)="b.MAT.2.9.2"> Kumbe ile nyota waliyokuwa wameiona upande wa mashariki iliwatangulia hata ikaenda kusimama juu ya mahali pale alipokuwa mtoto .

(src)="b.MAT.2.10.1"> فلما رأوا النجم فرحوا فرحا عظيما جدا .
(trg)="b.MAT.2.10.1"> Walipoiona hiyo nyota , walifurahi mno .

(src)="b.MAT.2.11.1"> وأتوا الى البيت ورأوا الصبي مع مريم امه . فخروا وسجدوا له . ثم فتحوا كنوزهم وقدموا له هدايا ذهبا ولبانا ومرّا .
(trg)="b.MAT.2.11.1"> Basi , wakaingia nyumbani , wakamwona yule mtoto pamoja na Maria mama yake ; wakapiga magoti , wakamsujudia .
(trg)="b.MAT.2.11.2"> Kisha wakafungua hazina zao , wakampa zawadi : dhahabu , ubani na manemane .

(src)="b.MAT.2.12.1"> ثم اذ أوحي اليهم في حلم ان لا يرجعوا الى هيرودس انصرفوا في طريق اخرى الى كورتهم
(trg)="b.MAT.2.12.1"> Mungu aliwaonya katika ndoto wasimrudie Herode ; hivyo wakarudi makwao kwa njia nyingine .

(src)="b.MAT.2.13.1"> وبعدما انصرفوا اذا ملاك الرب قد ظهر ليوسف في حلم قائلا قم وخذ الصبي وامه واهرب الى مصر وكن هناك حتى اقول لك . لان هيرودس مزمع ان يطلب الصبي ليهلكه .
(trg)="b.MAT.2.13.1"> Baada ya wale wageni kuondoka , malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto , akamwambia , " Amka !
(trg)="b.MAT.2.13.2"> Mchukue mtoto pamoja na mama yake , mkimbilie Misri .
(trg)="b.MAT.2.13.3"> Kaeni huko mpaka nitakapokwambia , maana Herode anakusudia kumwua huyu mtoto . "

(src)="b.MAT.2.14.1"> فقام واخذ الصبي وامه ليلا وانصرف الى مصر .
(trg)="b.MAT.2.14.1"> Hivyo , Yosefu aliamka , akamchukua mtoto pamoja na mama yake , akaondoka usiku , akaenda Misri .

(src)="b.MAT.2.15.1"> وكان هناك الى وفاة هيرودس . لكي يتم ما قيل من الرب بالنبي القائل من مصر دعوت ابني
(trg)="b.MAT.2.15.1"> Akakaa huko mpaka Herode alipokufa .
(trg)="b.MAT.2.15.2"> Jambo hilo lilifanyika ili neno alilosema Bwana kwa njia ya nabii litimie : " Nilimwita Mwanangu kutoka Misri . "

(src)="b.MAT.2.16.1"> حينئذ لما رأى هيرودس ان المجوس سخروا به غضب جدا . فارسل وقتل جميع الصبيان الذين في بيت لحم وفي كل تخومها من ابن سنتين فما دون بحسب الزمان الذي تحققه من المجوس .
(trg)="b.MAT.2.16.1"> Herode alipogundua kwamba wale wataalamu wa nyota walikuwa wamemhadaa , alikasirika sana .
(trg)="b.MAT.2.16.2"> Akaamuru watoto wote wa kiume mjini Bethlehemu na kandokando yake wenye umri wa miaka miwili na chini yake wauawe .
(trg)="b.MAT.2.16.3"> Alifanya hivyo kufuatana na muda aliopata kujua kutoka kwa wale wataalamu wa nyota .

(src)="b.MAT.2.17.1"> حينئذ تم ما قيل بارميا النبي القائل .
(trg)="b.MAT.2.17.1"> Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyosemwa kwa njia ya nabii Yeremia :

(src)="b.MAT.2.18.1"> صوت سمع في الرامة نوح وبكاء وعويل كثير . راحيل تبكي على اولادها ولا تريد ان تتعزى لانهم ليسوا بموجودين
(trg)="b.MAT.2.18.1"> " Sauti imesikika mjini Rama , kilio na maombolezo mengi .
(trg)="b.MAT.2.18.2"> Raheli anawalilia watoto wake , wala hataki kutulizwa , maana wote wamefariki . "

(src)="b.MAT.2.19.1"> فلما مات هيرودس اذا ملاك الرب قد ظهر في حلم ليوسف في مصر
(trg)="b.MAT.2.19.1"> Baada ya kifo cha Herode , malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri ,

(src)="b.MAT.2.20.1"> قائلا . قم وخذ الصبي وامه واذهب الى ارض اسرائيل . لانه قد مات الذين كانوا يطلبون نفس الصبي .
(trg)="b.MAT.2.20.1"> akamwambia , " Amka !
(trg)="b.MAT.2.20.2"> Mchukue mtoto pamoja na mama yake , urudi tena katika nchi ya Israeli , maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa . "

(src)="b.MAT.2.21.1"> فقام واخذ الصبي وامه وجاء الى ارض اسرائيل .
(trg)="b.MAT.2.21.1"> Basi , Yosefu aliamka , akamchukua mtoto pamoja na mama yake , akarejea katika nchi ya Israeli .

(src)="b.MAT.2.22.1"> ولكن لما سمع ان ارخيلاوس يملك على اليهودية عوضا عن هيرودس ابيه خاف ان يذهب الى هناك . واذ أوحي اليه في حلم انصرف الى نواحي الجليل .
(trg)="b.MAT.2.22.1"> Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake , aliogopa kwenda huko .
(trg)="b.MAT.2.22.2"> Naye baada ya kuonywa katika ndoto , alikwenda katika mkoa wa Galilaya ,

(src)="b.MAT.2.23.1"> وأتى وسكن في مدينة يقال لها ناصرة . لكي يتم ما قيل بالانبياء انه سيدعى ناصريا
(trg)="b.MAT.2.23.1"> akahamia katika mji uitwao Nazareti .
(trg)="b.MAT.2.23.2"> Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii : " Ataitwa Mnazare . "

(src)="b.MAT.3.1.1"> وفي تلك الايام جاء يوحنا المعمدان يكرز في برية اليهودية .
(trg)="b.MAT.3.1.1"> Siku hizo Yohane Mbatizaji alitokea , akaanza kuhubiri katika jangwa la Yudea :

(src)="b.MAT.3.2.1"> قائلا توبوا لانه قد اقترب ملكوت السموات .
(trg)="b.MAT.3.2.1"> " Tubuni , maana Ufalme wa mbinguni umekaribia . "

(src)="b.MAT.3.3.1"> فان هذا هو الذي قيل عنه باشعياء النبي القائل صوت صارخ في البرية اعدوا طريق الرب . اصنعوا سبله مستقيمة .
(trg)="b.MAT.3.3.1"> Huyu Yohane ndiye yule ambaye nabii Isaya alinena juu yake aliposema : " Sauti ya mtu imesikika jangwani : Mtayarishieni Bwana njia yake , nyoosheni vijia vyake . "

(src)="b.MAT.3.4.1"> ويوحنا هذا كان لباسه من وبر الابل وعلى حقويه منطقة من جلد . وكان طعامه جرادا وعسلا بريا .
(trg)="b.MAT.3.4.1"> Yohane alivaa vazi lililoshonwa kwa manyoya ya ngamia , na ukanda wa ngozi kiunoni mwake .
(trg)="b.MAT.3.4.2"> Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni .

(src)="b.MAT.3.5.1"> حينئذ خرج اليه اورشليم وكل اليهودية وجميع الكورة المحيطة بالاردن .
(trg)="b.MAT.3.5.1"> Basi , watu kutoka Yerusalemu , kutoka mkoa wote wa Yudea na sehemu zote za kandokando ya mto Yordani , walimwendea ,

(src)="b.MAT.3.6.1"> واعتمدوا منه في الاردن معترفين بخطاياهم
(trg)="b.MAT.3.6.1"> wakaziungama dhambi zao , naye akawabatiza katika mto Yordani .

(src)="b.MAT.3.7.1"> فلما رأى كثيرين من الفريسيين والصدوقيين ياتون الى معموديته قال لهم يا اولاد الافاعي من اراكم ان تهربوا من الغضب الآتي .
(trg)="b.MAT.3.7.1"> Lakini alipowaona Mafarisayo wengi na Masadukayo wanamjia ili awabatize , aliwaambia , " Enyi kizazi cha nyoka !
(trg)="b.MAT.3.7.2"> Ni nani aliyewadokezea kwamba mnaweza kuiepuka ghadhabu inayokuja ?

(src)="b.MAT.3.8.1"> فاصنعوا اثمارا تليق بالتوبة .
(trg)="b.MAT.3.8.1"> Onyesheni basi kwa matendo , kwamba mmetubu kweli .

(src)="b.MAT.3.9.1"> ولا تفتكروا ان تقولوا في انفسكم لنا ابراهيم ابا . لاني اقول لكم ان الله قادر ان يقيم من هذه الحجارة اولادا لابراهيم .
(trg)="b.MAT.3.9.1"> Msidhani kwamba mtaweza kujitetea kwa kusema , Baba yetu ni Abrahamu !
(trg)="b.MAT.3.9.2"> Nawaambieni hakika , Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu .

(src)="b.MAT.3.10.1"> والآن قد وضعت الفاس على اصل الشجر . فكل شجرة لا تصنع ثمرا جيدا تقطع وتلقى في النار .
(trg)="b.MAT.3.10.1"> Basi , shoka liko tayari kuikata mizizi ya miti ; hivyo , kila mti usiozaa matunda mazuri , utakatwa na kutupwa motoni .

(src)="b.MAT.3.11.1"> انا اعمدكم بماء للتوبة . ولكن الذي يأتي بعدي هو اقوى مني الذي لست اهلا ان احمل حذاءه . هو سيعمدكم بالروح القدس ونار .
(trg)="b.MAT.3.11.1"> Mimi ninawabatizeni kwa maji kuonyesha kwamba mmetubu .
(trg)="b.MAT.3.11.2"> Lakini yule anayekuja baada yangu ana uwezo kuliko mimi .
(trg)="b.MAT.3.11.3"> Mimi sistahili hata kubeba viatu vyake .
(trg)="b.MAT.3.11.4"> Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto .

(src)="b.MAT.3.12.1"> الذي رفشه في يده وسينقي بيدره ويجمع قمحه الى المخزن . واما التبن فيحرقه بنار لا تطفأ
(trg)="b.MAT.3.12.1"> Yeye anashika mkononi chombo cha kupuria nafaka , ili aipure nafaka yake ; akusanye ngano ghalani , na makapi ayachome kwa moto usiozimika . "

(src)="b.MAT.3.13.1"> حينئذ جاء يسوع من الجليل الى الاردن الى يوحنا ليعتمد منه .
(trg)="b.MAT.3.13.1"> Wakati huo Yesu alitoka Galilaya akafika katika mto Yordani , akamwendea Yohane ili abatizwe naye .

(src)="b.MAT.3.14.1"> ولكن يوحنا منعه قائلا انا محتاج ان اعتمد منك وانت تأتي اليّ .
(trg)="b.MAT.3.14.1"> Lakini Yohane alijaribu kumzuia akisema , " Je , wewe unakuja kwangu ?
(trg)="b.MAT.3.14.2"> Mimi hasa ndiye ninayehitaji kubatizwa nawe . "

(src)="b.MAT.3.15.1"> فاجاب يسوع وقال له اسمح الآن . لانه هكذا يليق بنا ان نكمل كل بر . حينئذ سمح له .
(trg)="b.MAT.3.15.1"> Lakini Yesu akamjibu , " Acha tu iwe hivyo kwa sasa , maana kwa namna hii inafaa tuyatekeleze yale yote Mungu anayotaka . "
(trg)="b.MAT.3.15.2"> Hapo Yohane akakubali .

(src)="b.MAT.3.16.1"> فلما اعتمد يسوع صعد للوقت من الماء . واذا السموات قد انفتحت له فرأى روح الله نازلا مثل حمامة وآتيا عليه .
(trg)="b.MAT.3.16.1"> Mara tu Yesu alipokwisha batizwa , alitoka majini ; na ghafla mbingu zikafunguka , akaona Roho wa Mungu akishuka kama njiwa na kutua juu yake .

(src)="b.MAT.3.17.1"> وصوت من السموات قائلا هذا هو ابني الحبيب الذي به سررت
(trg)="b.MAT.3.17.1"> Sauti kutoka mbinguni ikasema , " Huyu ndiye Mwanangu mpendwa , nimependezwa naye . "

(src)="b.MAT.4.1.1"> ثم أصعد يسوع الى البرية من الروح ليجرب من ابليس .
(trg)="b.MAT.4.1.1"> Kisha Roho alimwongoza Yesu mpaka jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi .

(src)="b.MAT.4.2.1"> فبعدما صام اربعين نهارا واربعين ليلة جاع اخيرا .
(trg)="b.MAT.4.2.1"> Akafunga siku arubaini mchana na usiku , na mwishowe akaona njaa .

(src)="b.MAT.4.3.1"> فتقدم اليه المجرب وقال له ان كنت ابن الله فقل ان تصير هذه الحجارة خبزا .
(trg)="b.MAT.4.3.1"> Basi , mshawishi akamjia , akamwambia , " Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu , amuru mawe haya yawe mikate . "

(src)="b.MAT.4.4.1"> فاجاب وقال مكتوب ليس بالخبز وحده يحيا الانسان بل بكل كلمة تخرج من فم الله .
(trg)="b.MAT.4.4.1"> Yesu akamjibu , " Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu : Binadamu hataishi kwa mikate tu , ila kwa kila neno asemalo Mungu . "

(src)="b.MAT.4.5.1"> ثم اخذه ابليس الى المدينة المقدسة واوقفه على جناح الهيكل .
(trg)="b.MAT.4.5.1"> Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu , mji mtakatifu , akamweka juu ya mnara wa hekalu ,

(src)="b.MAT.4.6.1"> وقال له ان كنت ابن الله فاطرح نفسك الى اسفل . لانه مكتوب انه يوصي ملائكته بك . فعلى اياديهم يحملونك لكي لا تصدم بحجر رجلك .
(trg)="b.MAT.4.6.1"> akamwambia , " Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu , jitupe chini ; maana imeandikwa : Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako ; watakuchukua mikononi mwao , usije ukajikwaa kwenye jiwe . "

(src)="b.MAT.4.7.1"> قال له يسوع مكتوب ايضا لا تجرب الرب الهك .
(trg)="b.MAT.4.7.1"> Yesu akamwambia , " Imeandikwa pia : Usimjaribu Bwana , Mungu wako . "

(src)="b.MAT.4.8.1"> ثم اخذه ايضا ابليس الى جبل عال جدا واراه جميع ممالك العالم ومجدها .
(trg)="b.MAT.4.8.1"> Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu , akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari zake ,

(src)="b.MAT.4.9.1"> وقال له اعطيك هذه جميعها ان خررت وسجدت لي .
(trg)="b.MAT.4.9.1"> akamwambia , " Hivi vyote nitakupa kama tu ukipiga magoti na kuniabudu . "

(src)="b.MAT.4.10.1"> حينئذ قال له يسوع اذهب يا شيطان . لانه مكتوب للرب الهك تسجد واياه وحده تعبد .
(trg)="b.MAT.4.10.1"> Hapo , Yesu akamwambia , " Nenda zako Shetani !
(trg)="b.MAT.4.10.2"> Imeandikwa : Utamwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake . "

(src)="b.MAT.4.11.1"> ثم تركه ابليس واذا ملائكة قد جاءت فصارت تخدمه
(trg)="b.MAT.4.11.1"> Basi , Ibilisi akamwacha , na malaika wakaja , wakamhudumia .

(src)="b.MAT.4.12.1"> ولما سمع يسوع ان يوحنا اسلم انصرف الى الجليل .
(trg)="b.MAT.4.12.1"> Yesu aliposikia kwamba Yohane ametiwa gerezani alikwenda Galilaya .

(src)="b.MAT.4.13.1"> وترك الناصرة واتى فسكن في كفرناحوم التي عند البحر في تخوم زبولون ونفتاليم .
(trg)="b.MAT.4.13.1"> Aliondoka Nazareti , akaenda Kafarnaumu , mji ulio kando ya bahari ya Genesareti , mpakani mwa wilaya za Zabuloni na Naftali , akakaa huko .

(src)="b.MAT.4.14.1"> لكي يتم ما قيل باشعياء النبي القائل .
(trg)="b.MAT.4.14.1"> Ndivyo lilivyotimia lile neno lililosemwa kwa njia ya nabii Isaya :

(src)="b.MAT.4.15.1"> ارض زبولون وارض نفتاليم طريق البحر عبر الاردن جليل الامم .
(trg)="b.MAT.4.15.1"> " Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali , kuelekea baharini ng ' ambo ya mto Yordani , Galilaya nchi ya watu wa Mataifa !

(src)="b.MAT.4.16.1"> الشعب الجالس في ظلمة ابصر نورا عظيما . والجالسون في كورة الموت وظلاله اشرق عليهم نور .
(trg)="b.MAT.4.16.1"> Watu waliokaa gizani wameona mwanga mkubwa .
(trg)="b.MAT.4.16.2"> Nao walioishi katika nchi ya giza na kivuli cha kifo , mwanga umewaangazia ! "

(src)="b.MAT.4.17.1"> من ذلك الزمان ابتدأ يسوع يكرز ويقول توبوا لانه قد اقترب ملكوت السموات
(trg)="b.MAT.4.17.1"> Tangu wakati huo Yesu alianza kuhubiri akisema , " Tubuni , maana ufalme wa mbinguni umekaribia ! "

(src)="b.MAT.4.18.1"> واذ كان يسوع ماشيا عند بحر الجليل ابصر اخوين سمعان الذي يقال له بطرس واندراوس اخاه يلقيان شبكة في البحر فانهما كانا صيادين .
(trg)="b.MAT.4.18.1"> Yesu alipokuwa anatembea kando ya ziwa Galilaya , aliwaona ndugu wawili wavuvi ; Simoni ( aitwae Petro ) na Andrea , ndugu yake ; walikuwa wakivua samaki kwa nyavu ziwani .

(src)="b.MAT.4.19.1"> فقال لهما هلم ورائي فاجعلكما صيادي الناس .
(trg)="b.MAT.4.19.1"> Basi , akawaambia , " Nifuateni , nami nitawafanya ninyi wavuvi wa watu . "

(src)="b.MAT.4.20.1"> فللوقت تركا الشباك وتبعاه .
(trg)="b.MAT.4.20.1"> Mara wakaziacha nyavu zao , wakamfuata .

(src)="b.MAT.4.21.1"> ثم اجتاز من هناك فرأى اخوين آخرين يعقوب بن زبدي ويوحنا اخاه في السفينة مع زبدي ابيهما يصلحان شباكهما فدعاهما .
(trg)="b.MAT.4.21.1"> Alipokwenda mbele kidogo , aliwaona ndugu wengine wawili : Yakobo na Yohane , wana wa Zebedayo .
(trg)="b.MAT.4.21.2"> Hao walikuwa ndani ya mashua pamoja na baba yao Zebedayo , wakitengeneza nyavu zao .
(trg)="b.MAT.4.21.3"> Basi Yesu akawaita ,

(src)="b.MAT.4.22.1"> فللوقت تركا السفينة واباهما وتبعاه
(trg)="b.MAT.4.22.1"> nao mara wakaiacha mashua pamoja na baba yao , wakamfuata .

(src)="b.MAT.4.23.1"> وكان يسوع يطوف كل الجليل يعلم في مجامعهم ويكرز ببشارة الملكوت ويشفي كل مرض وكل ضعف في الشعب .
(trg)="b.MAT.4.23.1"> Yesu alikuwa anakwenda kila mahali wilayani Galilaya , akifundisha katika masunagogi na kuhubiri Habari Njema juu ya ufalme wa Mungu .
(trg)="b.MAT.4.23.2"> Aliponya kila namna ya maradhi na magonjwa waliyokuwa nayo watu .

(src)="b.MAT.4.24.1"> فذاع خبره في جميع سورية . فاحضروا اليه جميع السقماء المصابين بامراض واوجاع مختلفة والمجانين والمصروعين والمفلوجين فشفاهم .
(trg)="b.MAT.4.24.1"> Habari zake zikaenea katika mkoa wote wa Siria .
(trg)="b.MAT.4.24.2"> Wagonjwa wote wenye maradhi ya kila namna na wale waliosumbuliwa na kila namna ya taabu : waliopagawa na pepo , wenye kifafa na watu waliokuwa wamelemaa , walipelekwa kwake ; naye akawaponya wote .

(src)="b.MAT.4.25.1"> فتبعته جموع كثيرة من الجليل والعشر المدن واورشليم واليهودية ومن عبر الاردن
(trg)="b.MAT.4.25.1"> Makundi mengi ya watu kutoka Galilaya , Dekapoli , Yerusalemu , Yudea na ng ' ambo ya mto Yordani , walimfuata .

(src)="b.MAT.5.1.1"> ولما رأى الجموع صعد الى الجبل . فلما جلس تقدم اليه تلاميذه .
(trg)="b.MAT.5.1.1"> Yesu alipoyaona makundi ya watu , alipanda mlimani , akaketi .
(trg)="b.MAT.5.1.2"> Wanafunzi wake wakamwendea ,

(src)="b.MAT.5.2.1"> ففتح فاه وعلمهم قائلا .
(trg)="b.MAT.5.2.1"> naye akaanza kuwafundisha :

(src)="b.MAT.5.3.1"> طوبى للمساكين بالروح . لان لهم ملكوت السموات .
(trg)="b.MAT.5.3.1"> " Heri walio maskini rohoni , maana ufalme wa mbinguni ni wao .

(src)="b.MAT.5.4.1"> طوبى للحزانى . لانهم يتعزون .
(trg)="b.MAT.5.4.1"> Heri walio na huzuni , maana watafarijiwa .

(src)="b.MAT.5.5.1"> طوبى للودعاء . لانهم يرثون الارض .
(trg)="b.MAT.5.5.1"> Heri walio wapole , maana watairithi nchi .

(src)="b.MAT.5.6.1"> طوبى للجياع والعطاش الى البر . لانهم يشبعون .
(trg)="b.MAT.5.6.1"> Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu , maana watashibishwa .

(src)="b.MAT.5.7.1"> طوبى للرحماء . لانهم يرحمون .
(trg)="b.MAT.5.7.1"> Heri walio na huruma , maana watahurumiwa .

(src)="b.MAT.5.8.1"> طوبى للانقياء القلب . لانهم يعاينون الله .
(trg)="b.MAT.5.8.1"> Heri wenye moyo safi , maana watamwona Mungu .

(src)="b.MAT.5.9.1"> طوبى لصانعي السلام . لانهم ابناء الله يدعون .
(trg)="b.MAT.5.9.1"> Heri wenye kuleta amani , maana wataitwa watoto wa Mungu .

(src)="b.MAT.5.10.1"> طوبى للمطرودين من اجل البر . لان لهم ملكوت السموات .
(trg)="b.MAT.5.10.1"> Heri wanaoteswa kwa sababu ya kufanya atakavyo Mungu , maana ufalme wa mbinguni ni wao .