# it/piccardo.xml.gz
# sw/barwani.xml.gz
(src)="s1.1"> In nome di Allah , il Compassionevole , il Misericordioso
(trg)="s1.1"> KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU .
(src)="s1.2"> La lode [ appartiene ] ad Allah , Signore dei mondi
(trg)="s1.2"> Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu , Mola Mlezi wa viumbe vyote ;
(src)="s1.3"> il Compassionevole , il Misericordioso ,
(trg)="s1.3"> Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu ;
(src)="s1.4"> Re del Giorno del Giudizio .
(trg)="s1.4"> Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo .
(src)="s1.5"> Te noi adoriamo e a Te chiediamo aiuto .
(trg)="s1.5"> Wewe tu tunakuabudu , na Wewe tu tunakuomba msaada .
(src)="s1.6"> Guidaci sulla retta via ,
(trg)="s1.6"> Tuongoe njia iliyo nyooka ,
(src)="s1.7"> la via di coloro che hai colmato di grazia , non di coloro che [ sono incorsi ] nella [ Tua ] ira , né degli sviati .
(trg)="s1.7"> Njia ya ulio waneemesha , siyo ya walio kasirikiwa , wala walio potea .
(src)="s2.1"> Alif , Lâm , Mîm .
(trg)="s2.1"> Alif Lam Mim .
(src)="s2.2"> Questo è il Libro su cui non ci sono dubbi , una guida per i timorati ,
(trg)="s2.2"> Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake ; ni uwongofu kwa wachamungu ,
(src)="s2.3"> coloro che credono nell' invisibile , assolvono all' orazione e donano di ciò di cui Noi li abbiamo provvisti ,
(trg)="s2.3"> Ambao huyaamini ya ghaibu na hushika Sala , na hutoa katika tuliyo wapa .
(src)="s2.4"> coloro che credono in ciò che è stato fatto scendere su di te e in ciò che è stato fatto scendere prima di te e che credono fermamente all' altra vita .
(trg)="s2.4"> Na ambao wanayaamini yaliyo teremshwa kwako , na yaliyo teremshwa kabla yako ; na Akhera wana yakini nayo .
(src)="s2.5"> Quelli seguono la guida del loro Signore ; quelli sono coloro che prospereranno .
(trg)="s2.5"> Hao wapo juu ya uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi , na hao ndio walio fanikiwa .
(src)="s2.6"> In verità [ per ] quelli che non credono , non fa differenza che tu li avverta oppure no : non crederanno .
(trg)="s2.6"> Hakika wale walio kufuru ni sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye , hawaamini .
(src)="s2.7"> Allah ha posto un sigillo sui loro cuori e sulle loro orecchie e sui loro occhi c'è un velo ; avranno un castigo immenso .
(trg)="s2.7.0"> Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao , na juu ya macho yao pana kifuniko .
(trg)="s2.7.1"> Basi watapata adhabu kubwa .
(src)="s2.8"> Tra gli uomini vi è chi dice : “ Crediamo in Allah e nel Giorno Ultimo !” e invece non sono credenti .
(trg)="s2.8"> Na katika watu , wako wasemao : Tumemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho , wala wao si wenye kuamini .
(src)="s2.9"> Cercano di ingannare Allah e coloro che credono , ma non ingannano che loro stessi e non se ne accorgono .
(trg)="s2.9"> Wanatafuta kumdanganya Mwenyezi Mungu na wale walio amini , lakini hawadanganyi ila nafsi zao ; nao hawatambui .
(src)="s2.10.0"> Nei loro cuori c'è una malattia e Allah ha aggravato questa malattia .
(trg)="s2.10.0"> Nyoyoni mwao mna maradhi , na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi .
(src)="s2.10.1"> Avranno un castigo doloroso per la loro menzogna .
(trg)="s2.10.1"> Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo .
(src)="s2.11"> E quando si dice loro : “ Non spargete la corruzione sulla terra” , dicono : “ Anzi , noi siamo dei conciliatori !” .
(trg)="s2.11.0"> Na wanapo ambiwa : Msifanye uharibifu ulimwenguni .
(trg)="s2.11.1"> Husema : Bali sisi ni watengenezaji .
(src)="s2.12.0"> Non sono forse questi i corruttori ?
(src)="s2.12.1"> Ma non se ne avvedono .
(trg)="s2.12"> Hakika wao ndio waharibifu , lakini hawatambui .
(src)="s2.13.0"> E quando si dice loro : “ Credete come hanno creduto gli altri uomini” , rispondono : “ Dovremmo credere come hanno creduto gli stolti ?” .
(trg)="s2.13.0"> Na wanapo ambiwa : Aminini kama walivyo amini watu .
(trg)="s2.13.1"> Husema : Tuamini kama walivyo amini wapumbavu ?
(src)="s2.13.1"> Non sono forse loro gli stolti ?
(src)="s2.13.2"> Ma non lo sanno .
(trg)="s2.13.2"> Hakika wao ndio wapumbavu , lakini hawajui tu .
(src)="s2.14"> Quando incontrano i credenti , dicono : “ Crediamo” ; ma quando sono soli con i loro dèmoni , dicono : “ Invero siamo dei vostri ; non facciamo che burlarci di loro” .
(trg)="s2.14.0"> Na wanapo kutana na walio amini husema : Tumeamini .
(trg)="s2.14.1"> Na wanapo kuwa peke yao na mashet'ani wao husema : Hakika sisi tu pamoja nanyi .
(src)="s2.15"> Allah si burla di loro , lascia che sprofondino nella ribellione , accecati .
(trg)="s2.15"> Mwenyezi Mungu atawadhihaki wao na atawawacha katika upotofu wao wakitangatanga ovyo .
(src)="s2.16.0"> Sono quelli che hanno scambiato la retta Guida con la perdizione .
(src)="s2.16.1"> Il loro è un commercio senza utile e non sono ben guidati .
(trg)="s2.16"> Hao ndio walio nunua upotofu kwa uwongofu ; lakini biashara yao haikupata tija , wala hawakuwa wenye kuongoka .
(src)="s2.17"> Assomigliano a chi accende un fuoco ; poi , quando il fuoco ha illuminato i suoi dintorni , Allah sottrae loro la luce e li abbandona nelle tenebre in cui non vedono nulla .
(trg)="s2.17"> Mfano wao ni kama mfano wa aliye koka moto , na ulipo tanda mwangaza wake kote kote Mwenyezi Mungu aliiondoa nuru yao na akawawacha katika giza , hawaoni .
(src)="s2.18"> Sordi , muti , ciechi , non possono ritornare .
(trg)="s2.18"> Viziwi , mabubu , vipofu ; kwa hivyo hawatarejea .
(src)="s2.19.0"> [ O come ] una nuvola di pioggia nel cielo , gonfia di tenebre , di tuoni e di fulmini : mettono le loro dita nelle orecchie temendo la morte a causa dei fulmini .
(trg)="s2.19.0"> Au ni kama mvua kubwa itokayo mbinguni , ina giza na radi na umeme ; wakawa wakitia vidole vyao masikioni mwao kwa ajili ya mingurumo , kwa kuogopa kufa .
(src)="s2.19.1"> E Allah accerchia i miscredenti .
(trg)="s2.19.1"> Na Mwenyezi Mungu amewazunguka makafiri .
(src)="s2.20.0"> Il lampo quasi li acceca : ogni volta che rischiara , procedono ; ma quando rimangono nell' oscurità si fermano .
(trg)="s2.20.0"> Unakaribia umeme kunyakua macho yao .
(trg)="s2.20.1"> Kila ukiwatolea mwangaza huenda , na unapo wafanyia giza husimama .
(src)="s2.20.1"> Se Allah avesse voluto , li avrebbe privati dell' udito e della vista .
(trg)="s2.20.2"> Na angelitaka Mwenyezi Mungu angeliondoa kusikia kwao na kuona kwao .
(src)="s2.20.2"> In verità Allah su tutte le cose è potente .
(trg)="s2.20.3"> Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu .
(src)="s2.21"> O uomini , adorate il vostro Signore Che ha creato voi e quelli che vi hanno preceduto , cosicché possiate essere timorati .
(trg)="s2.21.0"> Enyi watu !
(trg)="s2.21.1"> Muabuduni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu , ili mpate kuokoka .
(src)="s2.22.0"> [ Egli è ] Colui Che della terra ha fatto un letto e del cielo un edificio , e che dal cielo fa scendere l' acqua con la quale produce i frutti che sono il vostro cibo .
(trg)="s2.22.0"> ( Mwenyezi Mungu ) ambaye amekufanyieni hii ardhi kuwa kama tandiko , na mbingu kama paa , na akateremsha maji kutoka mbinguni , na kwayo akatoa matunda yawe riziki zenu .
(src)="s2.22.1"> Non attribuite consimili ad Allah ora che sapete .
(trg)="s2.22.1"> Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika , na hali nyinyi mnajua .
(src)="s2.23"> E se avete qualche dubbio in merito a quello che abbiamo fatto scendere sul Nostro Servo , portate allora una sura simile a questa e chiamate altri testimoni all' infuori di Allah , se siete veritieri .
(trg)="s2.23"> Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyo mteremshia mja wetu basi leteni sura moja ya mfano wake , na muwaite mashahidi wenu badala ya Mwenyezi Mungu , ikiwa mnasema kweli .
(src)="s2.24"> Se non lo fate - e non lo farete - temete il Fuoco , il cui combustibile sono gli uomini e le pietre , che è stato preparato per i miscredenti .
(trg)="s2.24"> Na mkitofanya - na wala hamtofanya kamwe - basi uogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe walio andaliwa hao wanao kanusha .
(src)="s2.25.0"> E annuncia a coloro che credono e compiono il bene , che avranno i Giardini in cui scorrono i ruscelli .
(src)="s2.25.1"> Ogni volta che sarà loro dato un frutto diranno : “ Già ci era stato concesso !” .
(trg)="s2.25.0"> Na wabashirie walio amini na wakatenda mema kwamba watapata mabustani yapitayo mito kati yake ; kila watapo pewa matunda humo , watasema : Haya ndiyo kama tuliyo pewa mbele .
(src)="s2.25.2"> Ma è qualcosa di simile che verrà loro dato ; avranno spose purissime e colà rimarranno in eterno .
(trg)="s2.25.1"> Na wataletewa matunda yaliyo fanana ; na humo watakuwa na wake walio takasika ; na wao humo watadumu .
(src)="s2.26.0"> In verità , Allah non esita a prendere ad esempio un moscerino o qualsiasi altra cosa superiore .
(trg)="s2.26.0"> Hakika Mwenyezi Mungu haoni haya kutoa mfano hata wa mbu na ulio wa zaidi yake .
(src)="s2.26.1"> Coloro che credono sanno che si tratta della verità che proviene dal loro Signore ; i miscredenti invece dicono : “ Cosa vuol dire Allah con un simile esempio ?” .
(trg)="s2.26.1"> Ama wale walio amini hujua ya kwamba hiyo ni haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi , lakini wale walio kufuru husema : Ni nini analo kusudia Mwenyezi Mungu kwa mfano huu ?
(src)="s2.26.2"> [ Con esso ] ne allontana molti , e molti ne guida .
(src)="s2.26.3"> Ma non allontana che gli iniqui ,
(trg)="s2.26.2"> Kwa mfano huu huwapoteza wengi na huwaongoa wengi ; lakini hawapotezi ila wale wapotovu ,
(src)="s2.27.0"> coloro che rompono il patto di Allah dopo averlo accettato , spezzano ciò che Allah ha ordinato di unire e spargono la corruzione sulla terra .
(src)="s2.27.1"> Quelli sono i perdenti .
(trg)="s2.27"> Wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha ifunga , na wakayakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu kuungwa , na wakafanya uharibifu katika nchi ; hao ndio wenye khasara .
(src)="s2.28.0"> Come potete essere ingrati nei confronti di Allah , quando eravate morti ed Egli vi ha dato la vita ?
(trg)="s2.28.0"> Vipi mnamkanusha Mwenyezi Mungu na hali mlikuwa wafu akakufufueni !
(src)="s2.28.1"> Poi vi farà morire e vi riporterà alla vita e poi a Lui sarete ricondotti .
(trg)="s2.28.1"> Kisha atakufisheni , tena atakufufueni , kisha kwake mtarejeshwa ? .
(src)="s2.29.0"> Egli ha creato per voi tutto quello che c'è sulla terra .
(trg)="s2.29.0"> Yeye ndiye aliye kuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi .
(src)="s2.29.1"> Poi si è rivolto al cielo e lo ha ordinato in sette cieli .
(trg)="s2.29.1"> Tena akazielekea mbingu , na akazifanya mbingu saba .
(src)="s2.29.2"> Egli è l' Onnisciente .
(trg)="s2.29.2"> Naye ndiye Mjuzi wa kila kitu .
(src)="s2.30.0"> E quando il tuo Signore disse agli Angeli : “ Porrò un vicario sulla terra” , essi dissero : “ Metterai su di essa qualcuno che vi spargerà la corruzione e vi verserà il sangue , mentre noi Ti glorifichiamo lodandoTi e Ti santifichiamo ?” .
(trg)="s2.30.0"> Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika : Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa ( mfwatizi ) , wakasema : Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu , hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako ?
(src)="s2.30.1"> Egli disse : “ In verità , Io conosco quello che voi non conoscete ...” .
(trg)="s2.30.1"> Akasema : Hakika Mimi nayajua msiyo yajua .
(src)="s2.31"> Ed insegnò ad Adamo i nomi di tutte le cose , quindi le presentò agli Angeli e disse : “ Ditemi i loro nomi , se siete veritieri” .
(trg)="s2.31"> Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote , kisha akaviweka mbele ya Malaika , na akasema : Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli .
(src)="s2.32.0"> Essi dissero : “ Gloria a Te .
(trg)="s2.32.0"> Wakasema : Subhanaka , Wewe umetakasika !
(src)="s2.32.1"> Non conosciamo se non quello che Tu ci hai insegnato : in verità Tu sei il Saggio , il Sapiente” .
(trg)="s2.32.1"> Hatuna ujuzi isipokuwa kwa uliyo tufunza Wewe .
(trg)="s2.32.2"> Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mwenye hikima .
(src)="s2.33.0"> Disse : “ O Adamo , informali sui nomi di tutte [ le cose ]” .
(trg)="s2.33.0"> Akasema : Ewe Adam !
(trg)="s2.33.1"> Waambie majina yake .
(src)="s2.33.1"> Dopo che li ebbe informati sui nomi , Egli disse : “ Non vi avevo forse detto che conosco il segreto dei cieli e della terra e che conosco ciò che manifestate e ciò che nascondete ?” .
(trg)="s2.33.2"> Basi alipo waambia majina yake alisema : Sikukwambieni kwamba Mimi ninajua siri za mbinguni na za duniani , na ninayajua mnayo yadhihirisha na mliyo kuwa mnayaficha ?
(src)="s2.34"> E quando dicemmo agli Angeli : “ Prosternatevi ad Adamo” , tutti si prosternarono , eccetto Iblîs , che rifiutò per orgoglio e fu tra i miscredenti .
(trg)="s2.34"> Na tulipo waambia Malaika : Msujudieni Adam , wakamsujudia wote isipo kuwa Iblis , alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri .
(src)="s2.35.0"> E dicemmo : “ O Adamo , abita il Paradiso , tu e la tua sposa .
(trg)="s2.35.0"> Na tulisema : Ewe Adam !
(src)="s2.35.1"> Saziatevene ovunque a vostro piacere , ma non avvicinatevi a quest' albero , ché in tal caso sareste tra gli empi” .
(trg)="s2.35.1"> Kaa wewe na mkeo katika Bustani , na kuleni humo maridhawa popote mpendapo , lakini msiukaribie mti huu tu ; mkawa katika wale walio dhulumu .
(src)="s2.36.0"> Poi Iblîs li fece inciampare e scacciare dal luogo in cui si trovavano .
(src)="s2.36.1"> E Noi dicemmo : “ Andatevene via , nemici gli uni degli altri .
(trg)="s2.36.0"> Lakini Shet'ani aliwatelezesha hao wawili na akawatoa katika waliyo kuwamo , na tukasema : Shukeni , nanyi ni maadui nyinyi kwa nyinyi .
(src)="s2.36.2"> Avrete una dimora sulla terra e ne godrete per un tempo stabilito” .
(trg)="s2.36.1"> Katika ardhi yatakuwa makaazi yenu na starehe kwa muda .
(src)="s2.37.0"> Adamo ricevette parole dal suo Signore e Allah accolse il suo [ pentimento ] .
(src)="s2.37.1"> In verità Egli è Colui Che accetta il pentimento , il Misericordioso .
(trg)="s2.37"> Kisha Adam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi , na Mola wake Mlezi alimkubalia toba yake ; hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba na Mwenye kurehemu .
(src)="s2.38.0"> Dicemmo : “ Andatevene via tutti [ quanti ] !
(src)="s2.38.1"> Se mai vi giungerà una guida da parte Mia , coloro che la seguiranno non avranno nulla da temere e non saranno afflitti” .
(trg)="s2.38"> Tukasema : Shukeni nyote ; na kama ukikufikieni uwongofu utokao kwangu , basi watakao fuata uwongofu wangu huo haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika .
(src)="s2.39"> E i miscredenti che smentiscono i Nostri segni , sono i compagni del Fuoco , in cui rimarranno per sempre .
(trg)="s2.39"> Na wenye kukufuru na kuzikanusha ishara zetu , hao ndio watakao kuwa watu wa Motoni , humo watadumu .
(src)="s2.40.0"> O figli di Israele , ricordate i favori di cui vi ho colmati e rispettate il Mio patto e rispetterò il vostro .
(src)="s2.40.1"> Solo Me dovete temere .
(trg)="s2.40.0"> Enyi Wana wa Israili !
(trg)="s2.40.1"> Kumbukeni neema yangu niliyo kuneemesheni , na timizeni ahadi yangu , na Mimi nitatimiza ahadi yenu , na niogopeni Mimi tu .
(src)="s2.41.0"> E credete in ciò che ho fatto scendere a conferma di quello che già era sceso su di voi e non siate i primi a rinnegarlo : non svendete i Miei segni per un prezzo vile .
(trg)="s2.41.0"> Na aminini niliyo yateremsha ambayo yanasadikisha mliyo nayo , wala msiwe wa kwanza kuyakataa .
(trg)="s2.41.1"> Wala msiuze Ishara zangu kwa thamani ndogo .
(src)="s2.41.1"> E temete soltanto Me .
(trg)="s2.41.2"> Na niogopeni Mimi tu .
(src)="s2.42"> E non avvolgete la verità di menzogna e non nascondete la verità ora che la conoscete .
(trg)="s2.42"> Wala msichanganye kweli na uwongo na mkaificha kweli nanyi mnajua .
(src)="s2.43"> E assolvete all' orazione , pagate la decima e inchinatevi con coloro che si inchinano .
(trg)="s2.43"> Na shikeni Sala , na toeni Zaka , na inameni pamoja na wanao inama .
(src)="s2.44.0"> Ordinerete ai popoli la carità e dimenticherete voi stessi , voi che leggete il Libro ?
(trg)="s2.44.0"> Je !
(trg)="s2.44.1"> Mnawaamrisha watu mema na mnajisahau nafsi zenu , na hali nyinyi mnasoma Kitabu ?
(src)="s2.44.1"> Non ragionate dunque ?
(trg)="s2.44.2"> Basi je , hamzingatii ?
(src)="s2.45"> Cercate aiuto nella pazienza e nell' adorazione , in verità essa è gravosa , ma non per gli umili
(trg)="s2.45"> Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kusali ; na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu ,
(src)="s2.46"> che pensano che invero incontreranno il loro Signore e che invero torneranno a Lui .
(trg)="s2.46"> Ambao wana yakini kuwa hakika watakutana na Mola wao Mlezi na ya kuwa hakika watarejea kwake .
(src)="s2.47"> O Figli di Israele , ricordate i favori di cui vi ho colmati e di come vi ho favorito sugli altri popoli del mondo .
(trg)="s2.47.0"> Enyi Wana wa Israili !
(trg)="s2.47.1"> Kumbukeni zile neema zangu nilizo kuneemesheni , na nikakuteuweni kuliko wote wengineo .
(src)="s2.48.0"> E temete il Giorno in cui nessun'anima potrà alcunché per un' altra , in cui non sarà accolta nessuna intercessione e nulla potrà essere compensato .
(src)="s2.48.1"> Essi non saranno soccorsi .
(trg)="s2.48"> Na iogopeni Siku ambayo mtu hatomfaa mtu kwa lolote , wala hayatakubaliwa kwake maombezi , wala hakitapokewa kikomboleo kwake ; wala hawatanusuriwa .
(src)="s2.49.0"> E [ ricordate ] quando vi abbiamo liberato dalla gente di Faraone che vi infliggeva le torture più atroci ! ...
(src)="s2.49.1"> Sgozzavano i vostri figli e lasciavano in vita le vostre femmine .
(src)="s2.49.2"> In ciò vi fu un' immensa prova da [ parte del ] vostro Signore .
(trg)="s2.49"> Na vile tulipo kuokoeni kwa watu wa Firauni walio kupeni adhabu mbaya , wakiwachinja wana wenu wa kiume na wakawawacha hai wanawake ; na katika hayo ulikuwa ni mtihani mkubwa ulio toka kwa Mola wenu Mlezi .
(src)="s2.50"> E quando abbiamo diviso il mare per voi , quindi vi abbiamo tratti in salvo e abbiamo annegato la gente di Faraone , mentre voi stavate a guardare .
(trg)="s2.50"> Na tulipo ipasua bahari kwa ajili yenu na tukakuokoeni , tukawazamisha watu wa Firauni , na huku mnatazama .
(src)="s2.51"> E quando stabilimmo con Mosè [ un patto in ] quaranta notti ... e voi vi prendeste il Vitello e agiste da iniqui .
(trg)="s2.51"> Na tulipo muahidi Musa masiku arubaini , kisha mkachukua ndama ( mkamuabudu ) baada yake , na mkawa wenye kudhulumu .
(src)="s2.52"> Ma Noi vi perdonammo : forse ne sareste stati riconoscenti .
(trg)="s2.52"> Kisha tukakusameheni baada ya hayo , ili mpate kushukuru .
(src)="s2.53"> E quando abbiamo dato a Mosè il Libro e il Discrimine : forse sarete ben guidati !
(trg)="s2.53"> Na tulipo mpa Musa Kitabu na pambanuo ili mpate kuongoka .
(src)="s2.54.0"> E quando Mosè disse al suo popolo : “ O popol mio , invero vi siete fatti un grande torto prendendovi il Vitello .
(trg)="s2.54.0"> Na Musa alipo waambia watu wake : Enyi watu wangu !
(trg)="s2.54.1"> Hakika nyinyi mmezidhulumu nafsi zenu kwa kuchukua kwenu ndama ( kumuabudu ) .
(src)="s2.54.1"> Pentitevi al vostro Creatore e datevi la morte : questa è la cosa migliore , di fronte al vostro Creatore” .
(trg)="s2.54.2"> Basi tubuni kwa Muumba wenu na ziueni nafsi zenu .
(trg)="s2.54.3"> Haya ni bora kwenu mbele ya Muumba wenu .
(src)="s2.54.2"> Poi Allah accolse il vostro [ pentimento ] .
(trg)="s2.54.4"> Naye akapokea toba yenu .
(src)="s2.54.3"> In verità Egli accoglie sempre [ il pentimento ] , è il Misericordioso
(trg)="s2.54.5"> Hakika Yeye ndiye apokeaye toba na Mwenye kurehemu .
(src)="s2.55.0"> E quando diceste : “ O Mosè , noi non ti crederemo finché non avremo visto Allah in maniera evidente” .
(trg)="s2.55.0"> Na mlipo sema : Ewe Musa !
(trg)="s2.55.1"> Hatutakuamini mpaka tumwone Mwenyezi Mungu waziwazi .
(src)="s2.55.1"> E la folgore vi colpì mentre stavate guardando .
(trg)="s2.55.2"> Ikakunyakueni radi nanyi mnaangalia .
(src)="s2.56"> Poi vi resuscitammo dalla morte : forse sarete riconoscenti .
(trg)="s2.56"> Kisha tukakufufueni baada ya kufa kwenu , ili mpate kushukuru .
(src)="s2.57.0"> E vi coprimmo con l' ombra di una nuvola , e facemmo scendere su di voi la manna e le quaglie : “ Mangiate queste delizie di cui vi abbiamo provvisti !” .
(trg)="s2.57.0"> Na tukakutilieni kivuli kwa mawingu na tukakuteremshieni Manna na Salwa ; tukakwambieni : Kuleni vitu vizuri hivi tulivyo kuruzukuni .
(src)="s2.57.1"> Non è a Noi che fecero torto , bensì a loro stessi .
(trg)="s2.57.1"> Nao hawakutudhulumu Sisi lakini walikuwa wanajidhulumu nafsi zao .
(src)="s2.58.0"> E quando dicemmo : “ Entrate in questa città e rifocillatevi dove volete a vostro piacimento ; ma entrate dalla porta inchinandovi e dicendo " perdono " .
(trg)="s2.58.0"> Na tulipo sema : Ingieni mji huu , na humo mle mpendapo maridhawa , na ingieni katika mlango wake kwa unyenyekevu , na semeni : Tusamehe !
(src)="s2.58.1"> Noi perdoneremo i vostri peccati ed aumenteremo coloro che avranno operato il bene” .
(trg)="s2.58.1"> Tutakusameheni makosa yenu , na tutawazidishia wema wafanyao wema .
(src)="s2.59.0"> Ma gli empi cambiarono la parola che era stata data loro .
(trg)="s2.59.0"> Lakini walio dhulumu waliibadili kauli isiyo kuwa waliyo ambiwa .
(src)="s2.59.1"> E facemmo scendere dal cielo un castigo sugli empi , per castigare la loro perversione .
(trg)="s2.59.1"> Kwa hivyo tukaiteremsha juu ya wale walio dhulumu adhabu kutoka mbinguni kwa sababu ya walivyo kuwa wamepotoka .
(src)="s2.60.0"> E quando Mosè chiese acqua per il suo popolo , dicemmo : “ Colpisci la roccia con il tuo bastone” .
(trg)="s2.60.0"> Na Musa alipo omba maji kwa ajili ya watu wake , tulimwambia : Lipige jiwe kwa fimbo yako .
(src)="s2.60.1"> E , improvvisamente , sgorgarono dodici fonti , e ogni tribù seppe dove doveva bere !
(trg)="s2.60.1"> Mara zikatimbuka chemchem kumi na mbili ; kila kabila ikajua mahali pake pa kunywea .
(src)="s2.60.2">“ Mangiate e bevete il sostentamento di Allah e non spargete la corruzione sulla terra .”
(trg)="s2.60.2"> Tukawaambia : Kuleni na mnywe riziki ya Mwenyezi Mungu , wala msiasi katika nchi mkafanya uharibifu .
(src)="s2.61.0"> E quando diceste : “ O Mosè , non possiamo più tollerare un unico alimento .
(src)="s2.61.1"> Prega per noi il tuo Signore che , dalla terra , faccia crescere per noi legumi , cetrioli , aglio , lenticchie e cipolle !” .
(trg)="s2.61.0"> Na mlipo sema : Ewe Musa !
(trg)="s2.61.1"> Hatuwezi kuvumilia chakula cha namna moja tu , basi tuombee kwa Mola wako Mlezi atutolee vile vinavyo mea katika ardhi , kama mboga zake , na matango yake , na thom zake , na adesi zake , na vitunguu vyake .
(src)="s2.61.2"> Egli disse : “ Volete scambiare il meglio con il peggio ?
(trg)="s2.61.2"> Akasema : Mnabadili kilicho duni kwa kilicho bora ?
(src)="s2.61.3"> Tornate in Egitto , colà troverete certamente quello che chiedete !” .
(trg)="s2.61.3"> Shukeni mjini , huko mtapata mlivyo viomba .
(src)="s2.61.4"> E furono colpiti dall' abiezione e dalla miseria e subirono la collera di Allah , perché dissimulavano i segni di Allah e uccidevano i profeti ingiustamente .
(trg)="s2.61.4"> Na wakapigwa na unyonge , na umasikini , na wakastahili ghadhabu ya Mwenyezi Mungu .
(trg)="s2.61.5"> Na haya ni kwa sababu walikuwa wakiyakataa maneno ya Mwenyezi Mungu , na wakiwauwa Manabii pasipo haki .