# en/ted2020-1.xml.gz
# sw/ted2020-1.xml.gz


(src)="1"> Thank you so much , Chris .
(trg)="1"> Ahsante sana Chris .

(src)="2"> And it 's truly a great honor to have the opportunity to come to this stage twice ; I 'm extremely grateful .
(trg)="2.1"> Pia kwakweli ni heshima kubwa kupata nafasi hii kuja katika ukumbi huu mara mbili .
(trg)="2.2"> Nashukuru kwa dhati .

(src)="3"> I have been blown away by this conference , and I want to thank all of you for the many nice comments about what I had to say the other night .
(trg)="3"> nimepigwa na butwaa na huu mkusanyiko , na nataka kuwapa shukrani kwa maoni mengi mazuri kuhusu niliyoongelea usiku ule .

(src)="4"> And I say that sincerely , partly because ( Mock sob ) I need that .
(trg)="4"> Ninasema hilo kwa dhati , kidogo kwasababu -- ( Kwikwi ya maskhara ) -- niliyahitaji !

(src)="5"> ( Laughter ) Put yourselves in my position .
(trg)="5"> ( Vicheko ) Jiweke katika nafasi yangu !

(src)="6"> ( Laughter ) I flew on Air Force Two for eight years .
(trg)="6"> Nilipaa kwa ndege " Air Force Two " kwa miaka nane .

(src)="7"> ( Laughter ) Now I have to take off my shoes or boots to get on an airplane !
(trg)="7"> Sasa inabidi nivue viatu vyangu au mabuti ili kupanda ndege .

(src)="8"> ( Laughter ) ( Applause ) I 'll tell you one quick story to illustrate what that 's been like for me .
(trg)="8"> ( Vicheko ) ( Makofi ) Nitawasimulia hadithi moja haraka kuonesha hali ilivyo kwangu .

(src)="9"> ( Laughter ) It 's a true story -- every bit of this is true .
(trg)="9"> Ni hadithi ya ukweli -- kila tukio ni ukweli .

(src)="10"> Soon after Tipper and I left the -- ( Mock sob ) White House -- ( Laughter ) we were driving from our home in Nashville to a little farm we have 50 miles east of Nashville .
(trg)="10"> Muda mfupi baada ya Tipper na mimi -- ( Kwikwi ya maskhara ) -- ( Vicheko ) -- tulikuwa tukiendesha gari kutoka nyumbani Nashville kwanda kwenye shamba letu dogo maili 50 mashariki mwa Nashville --

(src)="11"> Driving ourselves .
(trg)="11"> tukiendesha gari wenyewe .

(src)="12"> ( Laughter ) I know it sounds like a little thing to you , but -- ( Laughter ) I looked in the rear-view mirror and all of a sudden it just hit me .
(trg)="12"> Najua inasikika kama jambo dogo kwenu , lakini -- ( Vicheko ) -- Nikaangalia katika kioo cha kuangalizia nyuma na ghafla ikatokea nikagundua .

(src)="13"> There was no motorcade back there .
(trg)="13"> Kulikuwa hamna msafara huko nyuma .

(src)="14"> ( Laughter ) You 've heard of phantom limb pain ?
(trg)="14"> Mmesikia kuhusu maumivu ya phantom limb ?

(src)="15"> ( Laughter ) This was a rented Ford Taurus .
(trg)="15"> ( Vicheko ) Hili gari lilikuwa ni Ford Taurus ya kukodishwa .

(src)="16"> ( Laughter ) It was dinnertime , and we started looking for a place to eat .
(trg)="16"> Ilikuwa saa ya chakula cha jioni , na tukaanza kutafuta sehemu ya kupata chakula .

(src)="17"> We were on I-40 .
(trg)="17"> Tulikuwa katika barabara I-40 .

(src)="18"> We got to Exit 238 , Lebanon , Tennessee .
(trg)="18"> Tukaingia katika kona ya 238 , Lebanona , Tennessee .

(src)="19"> We got off the exit , we found a Shoney 's restaurant .
(trg)="19"> tukatoka katika hiyo barabara , tukaanza kutafua -- tukapata mgahawa wa Shoney .

(src)="20"> Low-cost family restaurant chain , for those of you who don 't know it .
(trg)="20"> Ni mnyonyoro wa migahawa inayomilikiwa na familia , kwa wale ambao hawaufahamu .

(src)="21"> We went in and sat down at the booth , and the waitress came over , made a big commotion over Tipper .
(trg)="21"> Tuliingia ndani na kukaa kibandani na muhudumu wa kike akaja , akafanya vurugu kubwa juu ya Tipper ( Vicheko )

(src)="22"> ( Laughter ) She took our order , and then went to the couple in the booth next to us , and she lowered her voice so much , I had to really strain to hear what she was saying .
(trg)="22"> Akachukua maagizo yetu , halafu akaenda kwa wawili waliokuwa kibanda kilichofuata , halafu alashusha sauti yake chini sana ilibidi nitumie juhudi nzito ili kusikia alichokuwa akisema .

(src)="23"> And she said " Yes , that 's former Vice President Al Gore and his wife , Tipper . "
(trg)="23"> Halafu akasema " Ndio , yule ni Makamu wa Raisi aliyepita Al Gore na Mkewe Tipper . "

(src)="24"> And the man said , " He 's come down a long way , hasn 't he ? "
(trg)="24"> Halafu huyo mwanaume akasema " Amekuja safari ndefu au sio ? "

(src)="25"> ( Laughter ) ( Applause ) There 's been kind of a series of epiphanies .
(trg)="25"> ( Vicheko ) Kumekuwa na kama mfululizo hivi wa kutokewa na ugunduzi ghafla .

(src)="26"> ( Laughter ) The very next day , continuing the totally true story , I got on a G-V to fly to Africa to make a speech in Nigeria , in the city of Lagos , on the topic of energy .
(trg)="26"> Siku iliyofuata , kuendeleza hadithi ya kweli kabisa , nilipanda G-5 kupaa mpaka Afrika kutoa hotuba Naijeria , jijini Lagos , kuhusu nishati .

(src)="27"> And I began the speech by telling them the story of what had just happened the day before in Nashville .
(trg)="27"> Na nikaanza hotuba kwa kuwaambia hii hadithi ya matukio ya siku ile jana yake kule Nashville .

(src)="28"> And I told it pretty much the same way I 've just shared it with you : Tipper and I were driving ourselves , Shoney 's , low-cost family restaurant chain , what the man said -- they laughed .
(trg)="28.1"> Na nilihadithia kama kwa namna hii hii nilivyoshikikishana na ninyi .
(trg)="28.2"> Tipper na mimi tulikuwa tukiendesha gari wenyewe , mgahawa wa gharama ndogo wa kifamilia wa Shoney , yale yule mwanaume alivyosema -- wakacheka .

(src)="29"> I gave my speech , then went back out to the airport to fly back home .
(trg)="29"> Nikatoa hotuba yangu , halafu nikarudi uwanja wa ndege kurudi nyumbani .

(src)="30"> I fell asleep on the plane until , during the middle of the night , we landed on the Azores Islands for refueling .
(trg)="30"> Niliishia usingizini kwenye ndege , mpaka usiku wa manane , tulitua visiwa nya Azores kwa ajili ya kuongeza mafuta .

(src)="31"> I woke up , they opened the door , I went out to get some fresh air , and I looked , and there was a man running across the runway .
(trg)="31"> Nikaamka , wakafungua mlango , nikatoka nje kupata hewa safi kidogo , halafu nikaangalia na nikamuona mwanaume akikimbia katika barabara ya ndege .

(src)="32.1"> And he was waving a piece of paper , and he was yelling , " Call Washington !
(src)="32.2"> Call Washington ! "
(trg)="32.1"> Alikua akipunga kipande cha karatasi na alikuwa akipayuka , " Piga simu Washington !
(trg)="32.2"> Piga simu Washington ! "

(src)="33"> And I thought to myself , in the middle of the night , in the middle of the Atlantic , what in the world could be wrong in Washington ?
(trg)="33.1"> Halafu nikafikiria , usiku wa manane , katikati ya Atlantic , kuna kasoro gani duniani huko Washington ?
(trg)="33.2"> Halafu nikakumbuka inaweza ikawa ni rundo la maswala .

(src)="34"> Then I remembered it could be a bunch of things .
(trg)="34"> ( Vicheko )

(src)="35"> ( Laughter ) But what it turned out to be , was that my staff was extremely upset because one of the wire services in Nigeria had already written a story about my speech , and it had already been printed in cities all across the United States of America .
(trg)="35.1"> Lakini kumbe ilikuwa kwamba wafanyakazi wangu walikuwa wamechukizwa sana kwasababu moja huduma za habari kule Naijeria ilikuwa tayari imeandika habari kuhusu hotuba yangu .
(trg)="35.2"> Halafu ilikuwa tayari imeshachapishwa kwenye miji kote Marekani

(src)="36"> It was printed in Monterey , I checked .
(trg)="36"> -- ilichapishwa Monterey , nilihakikisha .

(src)="37.1"> ( Laughter ) And the story began , " Former Vice President Al Gore announced in Nigeria yesterday , " quote : ' My wife Tipper and I have opened a low-cost family restaurant ' " -- ( Laughter ) " ' named Shoney 's , and we are running it ourselves . ' "
(src)="37.2"> ( Laughter ) Before I could get back to U.S. soil , David Letterman and Jay Leno had already started in on -- one of them had me in a big white chef 's hat , Tipper was saying , " One more burger with fries ! "
(trg)="37.1"> Halafu habari zikaanza , " Makamu wa Raisi aliyepita Al Gore ametangaza Naijeria jana , " Mke wangu Tipper na mimi tumefungua mgahawa wa kifamilia wa gharama za chini uitwao Shoney 's , na tunauendesha wenyewe .
(trg)="37.2"> ' ' ' ( Vicheko ) Kabla sijafika katika ardhi ya Marekani , David Letterman na Jay Leno walikuwa wameshalianzia hili -- mmoja wao aliniweka katika kofia kubwa ya mpishi , Tipper alikuwa akisema " Burger moja ya nyongeza na chipsi ! "

(src)="38"> ( Laughter ) Three days later , I got a nice , long , handwritten letter from my friend and partner and colleague Bill Clinton , saying , " Congratulations on the new restaurant , Al ! "
(trg)="38"> Siku tatu baadae , nikapokea barua nzuri , ndefu , iliyoandikwa na mkono kutoka kwa rafiki yangu mpenzi na mfanyakazi mwenza Bill Clinton akisema , " Hongera kwa mgahawa mpya , Al ! "

(src)="39"> ( Laughter ) We like to celebrate each other 's successes in life .
(trg)="39"> ( Vicheko ) Tunapenda kusheherekea mafanikio yetu na ya wenzetu maishani .

(src)="40"> ( Laughter ) I was going to talk about information ecology .
(trg)="40"> Nilikuwa niongelee ikolojia ya habari .

(src)="41"> But I was thinking that , since I plan to make a lifelong habit of coming back to TED , that maybe I could talk about that another time .
(trg)="41"> Lakini nilifikiria kwamba sababu nilipanga kuwa na tabia ya kuja tena TED , kwamba labda ningeongelea hilo wakati mwingine ( Makofi )

(src)="42"> ( Applause ) Chris Anderson : It 's a deal !
(trg)="42"> Chris Anderson : Ni mpango !

(src)="43"> ( Applause ) Al Gore : I want to focus on what many of you have said you would like me to elaborate on : What can you do about the climate crisis ?
(trg)="43.1"> Al Gore : Nataka kulenga kwenye ambalo wengi wenu mmesema mnataka nilifafanue .
(trg)="43.2"> Ni nini ambacho unaweza kufanya kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ?

(src)="44"> I want to start with a couple of -- I 'm going to show some new images , and I 'm going to recapitulate just four or five .
(trg)="44"> Nataka nianze na -- Nitawaonesha picha kadhaa mpya , na nitafupisha maelezo kwenda nne au tano tu .

(src)="45"> Now , the slide show .
(trg)="45.1"> Sasa maonesho .
(trg)="45.2"> Naongeza upya wa maonesho haya kila wakati ninapoyafanya .

(src)="47"> I add new images , because I learn more about it every time I give it .
(trg)="46"> Naongeza picha mpya kwasababu najifunza zaidi kuhusu hili swala kila wakati ninapoonesha .

(src)="48"> It 's like beach-combing , you know ?
(trg)="47"> ni kama uokotaji fukweni , unajua ?

(src)="49"> Every time the tide comes in and out , you find some more shells .
(trg)="48"> Kila wakati wimbi lijapo na linapoondoka , unapata vifuniko vya chaza zaidi .

(src)="50"> Just in the last two days , we got the new temperature records in January .
(trg)="49"> Ndani ya siku mbili tu zilizopita , tumepata rekodi mpya za joto za mwezi wa kwanza .

(src)="51"> This is just for the United States of America .
(trg)="50"> Hizi ni za Marekani tu .

(src)="52"> Historical average for Januarys is 31 degrees ; last month was 39.5 degrees .
(trg)="51"> Wastani wa kihistoria wa mwezi wa kwanza ni digrii 31 . mwezi uliopita ilikuwa digrii 39.5 .

(src)="53"> Now , I know that you wanted some more bad news about the environment -- I 'm kidding .
(trg)="52"> Sasa , najua mlitaka habari mbaya zaidi kuhusu mazingira -- natania -- lakini haya maonesho ni ufupisho ,

(src)="54"> But these are the recapitulation slides , and then I 'm going to go into new material about what you can do .
(trg)="53"> halafu nitaingia katika maelezo mapya kuhusu mtachowezafanya .

(src)="55"> But I wanted to elaborate on a couple of these .
(trg)="54"> Lakini nilitaka kufafanua mawili ya haya .

(src)="56"> First of all , this is where we 're projected to go with the U.S. contribution to global warming , under business as usual .
(trg)="55"> Kwanza , hapa ndipo tunapotabiriwa kwenda katika mchango wa Marekani kwenye mabadiliko ya hali ya hewa , katika biashara kama kawaida .

(src)="57"> Efficiency in end-use electricity and end-use of all energy is the low-hanging fruit .
(trg)="56"> Ufanisi katika matumizi ya mwisho ya umeme na matumizi ya mwisho ya nishati yote ni tunda lining 'inialo karibu na chini .

(src)="58"> Efficiency and conservation -- it 's not a cost ; it 's a profit .
(trg)="57.1"> Ufanisi na uhifadhi .
(trg)="57.2"> Hli sio gharama , ni faida.Hii bango sio sahihi .

(src)="60"> It 's not negative ; it 's positive .
(trg)="58"> Sio hasi , ni chanya .

(src)="61"> These are investments that pay for themselves .
(trg)="59"> Huu ni uwekezaji ujaojilipia wenyewe .

(src)="62"> But they are also very effective in deflecting our path .
(trg)="60"> Lakini pia ni wafanisi sana katika kupotosha njia yetu .

(src)="63"> Cars and trucks -- I talked about that in the slideshow , but I want you to put it in perspective .
(trg)="61"> Magari na malori -- Niliongelea kuhusu hilo kwenye yale maonesho ya picha , lakini nawataka ninyi myaweke katika mtazamo .

(src)="64"> It 's an easy , visible target of concern -- and it should be -- but there is more global warming pollution that comes from buildings than from cars and trucks .
(trg)="62"> Ni rahisi , na ni lengo lionekanalo lenye wasiwasi , na linatakiwa kuwa hivyo , lakini kuna mabadiliko ya hali ya hewa ya uchafuzi ambayo yanatokana na majengo kuliko yanayotokana na magari na malori .

(src)="65"> Cars and trucks are very significant , and we have the lowest standards in the world .
(trg)="63"> Magari na malori ni muhimu , na tuna viwango vya chini kabisa duniani ,

(src)="66.1"> And so we should address that .
(src)="66.2"> But it 's part of the puzzle .
(trg)="64.1"> kwahiyo tunatakiwa kujaribu tatua hilo .
(trg)="64.2"> Lakini ni sehemu ya kitendawili hiki .

(src)="67"> Other transportation efficiency is as important as cars and trucks .
(trg)="65"> Ufanisi wa usafiri mwingine ni muhimu kama magari ya abiria na ya mizigo !

(src)="68"> Renewables at the current levels of technological efficiency can make this much difference .
(trg)="66"> Vyanzo vijizalilishaji katika viwango vya sasa vya ufanisi wa kiteknolojia vinaweza kuleta tofauti kiasi hiki , na pakiwa na waliyofanya Vinod na John Doerr na wengineo ,

(src)="69"> And with what Vinod , and John Doerr and others , many of you here -- there are a lot of people directly involved in this -- this wedge is going to grow much more rapidly than the current projection shows it .
(trg)="67"> wengi wenu mlio hapa -- wengi wanahusika moja kea moja na hili -- hili tatizo litakuwa kwa kasi zaidikuliko makadirio ya sasa yanavyoonesha .

(src)="70"> Carbon Capture and Sequestration -- that 's what CCS stands for -- is likely to become the killer app that will enable us to continue to use fossil fuels in a way that is safe .
(trg)="68"> Carbon capture and sequestation -- ndio CCS inavyosimama badala yake ina uwezekano wa kuwa utumizi muhimu mkuu hiyo itatuwezesha sisi kuendelea kutumia mafuta asili kwa namna mbayo ni salama .

(src)="71"> Not quite there yet .
(trg)="69"> Lakini bado kidogo .

(src)="72.1"> OK .
(src)="72.2"> Now , what can you do ?
(trg)="70.1"> Sawa .
(trg)="70.2"> Sasa , ninyi mfanye nini ?
(trg)="70.3"> Punguza uzalishaji wa hewa chafu majumbani .

(src)="74"> Most of these expenditures are also profitable .
(trg)="71"> Nyingi ya hizi gharama zinazalisha faida pia .

(src)="75"> Insulation , better design .
(trg)="72"> Kupunguza upotevu wa joto , ubunifu bora , ununuzi wa umeme bora kimazingira pale iwezekanapo .

(src)="77"> I mentioned automobiles -- buy a hybrid .
(trg)="73"> Nimegusia magari -- nunua yatumiayo mchanganyo .

(src)="78"> Use light rail .
(trg)="74"> Tumia reli nyepesi .

(src)="79"> Figure out some of the other options that are much better .
(trg)="75"> Tafuta machaguo kadhaa mengine ambayo ni mazuri zaidi .

(src)="80"> It 's important .
(trg)="76"> Ni muhimu .

(src)="81"> Be a green consumer .
(trg)="77"> Kuwa mtumiaji rafiki kimazingira .

(src)="82"> You have choices with everything you buy , between things that have a harsh effect , or a much less harsh effect on the global climate crisis .
(trg)="78"> Una machaguo katika kila ununuacho , baina ya vitu vyenye athari kali au athari ndogo zaidi kwenye mabadiliko ya hali ya hewa duniani .

(src)="83"> Consider this : Make a decision to live a carbon-neutral life .
(trg)="79.1"> Fikiria hili .
(trg)="79.2"> Chagua kuishi maisha yasiyokuwa na kaboni .

(src)="84"> Those of you who are good at branding , I 'd love to get your advice and help on how to say this in a way that connects with the most people .
(trg)="80"> Kwa wale kati yenu ambao ni madhubuti katika usanifu wa majina , ningependa kupata ushauri na msaada wenu katika namna ya kusema hili kwa namna ambayo inapatana na watu wengi .

(src)="85"> It is easier than you think .
(trg)="81"> Ni rahisi kuliko unavyofikiri .

(src)="86"> It really is .
(trg)="82"> Kweli kabisa .

(src)="87"> A lot of us in here have made that decision , and it is really pretty easy .
(trg)="83"> Wengi wetu humu tumefanya huo uamuzi na ni rahisi tu .

(src)="88"> It means reduce your carbon dioxide emissions with the full range of choices that you make , and then purchase or acquire offsets for the remainder that you have not completely reduced .
(trg)="84"> punguza uzalishaji wako wa kaboni daioksaidi kwa kutumia machaguo yako mbalimbali halafu nunuaau pata jinsi za kukabiliana kwa ajili ya kiasi kilichobaki pasipokupungua kabisa .

(src)="89"> And what it means is elaborated at climatecrisis.net .
(trg)="85"> Na ufafanuzi wa haya unapatikala climatecrisis.net .

(src)="90"> There is a carbon calculator .
(trg)="86"> Hapo pana kikokotozi cha kaboni .

(src)="91"> Participant Productions convened -- with my active involvement -- the leading software writers in the world , on this arcane science of carbon calculation , to construct a consumer-friendly carbon calculator .
(trg)="87"> washiriki wazalishaji walikusanyika , pakiwa na uhusika hai kutoka kwangu , waandishi viongozi duniani wa programu za kompyuta katika hii sayansi geni ya ukokotozi wa kaboni kujenga kikokotozi cha kaboni ambacho ni rafiki kwa mtumiaji .

(src)="92"> You can very precisely calculate what your CO2 emissions are , and then you will be given options to reduce .
(trg)="88"> unaweza kwa usahii wa hali yuu kukokotoa kiasi cha utoaji wako wa CO2 , halafu ndipo utapewa machaguo yenyekupunguza .

(src)="93"> And by the time the movie comes out in May , this will be updated to 2.0 , and we will have click-through purchases of offsets .
(trg)="89"> Na wakati filamu inapokaribia kuzinduliwa Mei , hii kuongezwa kuwa 2.0 na sisi tutabidi tubonye kununua jinsi za kukabiliana .

(src)="94"> Next , consider making your business carbon-neutral .
(trg)="90"> Linalofuata , fikiria kuifanya biashara yako isiwe itoayo kaboni .

(src)="95"> Again , some of us have done that , and it 's not as hard as you think .
(trg)="91"> Tena , baadhi yetu tumeshafanya hivyo , na sio vigumu kama unavyofikiri .

(src)="96"> Integrate climate solutions into all of your innovations , whether you are from the technology , or entertainment , or design and architecture community .
(trg)="92"> Unganisha ufumbuzi wa maswala hali ya hewa katika maswala yako yote ya uvumbuzi , kama unatoka katika maeneo ya teknolojia au burudani , au ubunifu na usanifumajengo .

(src)="97"> Invest sustainably .
(trg)="93"> Wekeza kwa uendelevu .

(src)="98"> Majora mentioned this .
(trg)="94"> Majora alidokeza hili .

(src)="99"> Listen , if you have invested money with managers who you compensate on the basis of their annual performance , don 't ever again complain about quarterly report CEO management .
(trg)="95"> Sikiliza , kawa umewekeza fedha na mameneja ambao unawapa fidia kutakana na matokeo wanayoonesha kwa mwaka , usilalamike tena kuhusu taarifa za kila robomwaka za usimamizi wa mkurugenzi mtendaji .

(src)="100"> Over time , people do what you pay them to do .
(trg)="96"> Baada ya muda , Watu wanafanya kile unachewalipa ili wafanye .

(src)="101"> And if they judge how much they 're going to get paid on your capital that they 've invested , based on the short-term returns , you 're going to get short-term decisions .
(trg)="97"> Na kama wataamua kiasi gani watalipwa kutoka mtaji wako ambao wamewekeza , kutokana na faida za ndani ya muda mfupi , utapata maamuzi ya ndani ya muda mfupi .

(src)="102"> A lot more to be said about that .
(trg)="98"> Kuna mengi ya kusemwa kuhusu hilo .

(src)="103"> Become a catalyst of change .
(trg)="99"> Kuwa kichocheo cha mabadiliko .

(src)="104"> Teach others , learn about it , talk about it .
(trg)="100"> Wafundishe wengine , jifunze kuhusu hayo , yaongelee .