# he/2016_10_15_409_.xml.gz
# sw/2016_10_mfungwa-wa-zamani-wa-guantanamo-ahatarisha-maisha-yake-kwa-kugoma-kula-akishinikiza-kuunganishwa-na-familia-yake_.xml.gz


(src)="1.1"> אסיר לשעבר בגואנטאנמו נמצא בסכנת מוות בעקבות שביתת רעב בה פתח בנסיון להתאחד עם משפחתו
(trg)="1.1">Mfungwa wa Zamani wa Guantanamo Ahatarisha Maisha Yake Kwa Kugoma Kula Akishinikiza Kuunganishwa na Familia Yake

(src)="1.2"> ג ׳ יהאד דיאב יזדקק לקביים לשארית חייו-מזכרת תמידית מהעינוי שעבר במשך 12 שנים , 8 חודשים ושבוע כאסיר במפרץ גואנטאנמו , בית הכלא המתופעל על ידי הצבא האמריקאי לשם החזקת חשודים בפשעי מלחמה בלי הגבלת זמן וללא משפט .
(trg)="1.2">Jihad Diyab atahitaji magongo ya kutembelea kwa maisha yake yote yakiwa ni kitu cha kumkumbusha mateso aliyoyavumilia kwa miaka 12, miezi 8 na siku 7 kama mfungwa katika gereza la Guantanamo Bay, mahali ambapo jeshi la Marekani lilikuwa likiendesha gereza likiweka washukiwa wa makosa ya kivita kwa muda usiofahamika na bila kufunguliwa mashtaka.

(src)="2.2"> בריאיון מוקדם יותר השנה באורוגוואי , הוא סיפר לעיתונאי ארגנטינאי שגואנטאנמו פוקד את האסירים ״ שהתמזל מזלם לעזוב .
(trg)="2.2">Katika mahojiano yaliyafanyika mapema mwaka huu huko Uruguai, alimwambia an mwandishi wa Ki-Agentina kuwa jinamizi la Guantanamo bado linawawinda hata wafungwa waliokuwa na bahati ya kuondoka mahali hapo.

(src)="2.3"> אלה שיוצאים עדיין אסירים של ארה ״ ב בנפשם ״ הוא אמר .
(trg)="2.3">Anasema kuwa "wote waliofanikiwa kutoka humo bado ni wafungwa wa Marekani kwa ndani"

(src)="3.1"> דיאב הוא אחד משישה אסירים ( ארבעה סורים , פלשתינאי , ותוניסאי ) ששוחררו מגואנטאנמו ועברו לאורוגוואי בדצמבר 2014 , בעקבות הסכם בין נשיא ארה ״ ב ברק אובאמה ונשיא אורוגוואי חוזה ״ פפה ״ מוחיקה .
(trg)="3.1">Diyab ni kati ya wafungwa sita kutoka Guantanamo ( Wasyria wanne, Mpalestina mmoja na Mtunisia mmoja) ambao waliachiliwa huru na kukaribishwa nchini Uruguai hapo Disemba 2014,shukrani kwa serikali iliyofanya makubaliano kati ya Rais wa Marekani Barack Obama na Rais wa Uruguai José “Pepe” Mujica.

(src)="4.1"> בעקבות נסיון כושל להתאחד עם משפחתו , שברחה מסוריה לתורכיה , דיאב הכריז על שביתת רעב באמצע אוגוסט .
(trg)="4.1">Kufuatia kushindwa kwa jitihada za kuungana na familia yake, iliyokimbia kutoka Syria kwenda Uturuki, Diyab alitangaza mgomo wa kula katikati mwa mwezi Agosti.

(src)="4.3"> הבריאות שלי לא יציבה .
(trg)="4.3">Hali ya afya yangu kwa sasa ni mbaya sana.

(src)="4.5"> בסוף ספטמבר , אחרי שהובטח לו שמשפחתו בטוחה בתורכיה , הוא פתח בדיאטת נוזלים .
(trg)="4.5">Mwishoni mwa Septemba, baada ya kupokea uhakika wa kuwa familia yake iko salama huko Uturuki, alianza tena kula vyakula vya majimaji .

(src)="5.1"> דיאב הגיע לכותרות ביוני האחרון , כשברח מאורוגוואי אל ברזיל .
(trg)="5.1">Diyab alitengeneza vichwa vya habari mwezi Juni, alipokimbia Uruguai kupitia mpaka wa Brazili.

(src)="5.2"> התקשורת באורוגוואי קראה לו ״ מורד כפוי טובה ״ על שעזב מדינה שקיבלה אותו לאחר השבי בארה ״ ב .
(trg)="5.2">Vyombo vya habari vya Uruguai vilimuita "muasi asiye na shukrani" kwa kuikimbia nchi iliyompokea kutoka utumwa wa Marekani.

(src)="5.3"> לאחר חודש של אי-וודאות לגבי מקום הימצאו , דיאב אותר בקרקאס , ונצואלה , שם עוכב ל-17 יום ואז גורש בחזרה למונטיווידאו .
(trg)="5.3">Baada ya mwezi usio na matumaini kuhusu mwenendo wake, Diyab aliibukia katika mji wa Caracas nchini Venezuela, ambapo alikamatwa na kuswekwa ndani na hatimaye kusafirishwa tena kwenda Montevideo.

(src)="7.1"> לפי העיתון ברכה , למרות הכחשותיהם של בכירי ממשל באורוגוואי , נראה שאורוגוואי הסכימה לדרוש שהאסירים המשוחררים יישארו במדינה למשך שנתיים לפני שהם עוברים אל מחוץ למדינה .
(trg)="7.1">Kulingana na gazeti la Brecha,Uruguai inaonekana kukubali kuwachukua wafungwa walioachiliwa huru na kuwaweka nchini kwa miaka miwili kabla ya kutoa mguu nje ya nchi hiyo, ingawa maafisa wa serikali ya Uruguai wanakataa kuwa waliafikiana na taratibu hizo.

(src)="9.1"> כיום , דעת הציבור לגבי אסירים משוחררים מגואנטאנמו שונה , ואפילו נשיא אורוגוואי לשעבר שנשא ונתן את שחרור האסירים אומר כעת שקבלת האסירים היתה המחיר שארצו היתה צריכה לשלם כדי להמשיך ״ למכור תפוזים לארצות הברית ״ ולשמור על קשרים טובים בין המדינות .
(trg)="9.1">Leo, mtazamo wa jamii kuhusu wafungwa wa zamani wa Guantanamo umebadilika na hata raisi wa zamani wa Uruguai aliyejadili kuhusu uhuru wa wafungwa hao kwa sasa anasema kuwa, kuwapokea hao watu ilikuwa ndio gharama nchi yake ilipaswa kulipa ili iweze kuendelea "kuuza machungwa nchini Marekani" na kuimarisha mahusiano mema.

(src)="10.1"> מחאת האסירים
(trg)="9.2">Maandamano ya Wafungwa

(src)="11.1"> חמישה חודשים אחרי שהגיעו לאורוגוואי , ארבעה מתוך ״ השישה מגואנטאנמו ״ מחו לפני שגרירות ארה ״ ב במונטיווידאו .
(trg)="9.3">Miezi mitano baada ya kuwasili nchini Uruguai wafungwa wanne kati ya "sita kutoka Guantanamo" walifanya maandamano mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Montevideo.

(src)="11.2"> דיאב לא היה נוכח .
(trg)="9.4">Diyab hakuwepo.

(src)="11.3"> הגברים התאספו לאחר ששמעו שוואשינגטון סירבה לספק להם תמיכה כלכלית .
(trg)="9.5">Wanaume hao walijikusanya mahali hapo baada ya kugundua kuwa Marekani imekataa kuwapa msaada wa fedha.

(src)="12.1"> בבלוג , הגברים כתבו שהם הושלכו למדינה זרה ללא תעסוקה , בלי משפחותיהם , ובלי ידע בשפה המקומית .
(trg)="10.1">Wakiandika katika blogu,wanaume hao wanasema kuwa wametelekezwa katika nchi ya kigeni bila ajira, bila familia zao au uelewa wa lugha ya asili ya mahali hapo.

(src)="12.4"> הם צריכים לספק לנו אמצעים לחיות כבני אדם מן השורה .
(trg)="10.4">Hawawezi kurusha makosa kwa watu wengine, wangetusaidia nyumba na misaada ya kifedha.

(src)="12.7"> אנחנו חושבים שזה הכי פחות שהם יכולים לעשות או אנחנו יכולים לבקש
(trg)="10.6">Tunafikiri kuwa hiki ni kitu kidogo tu wanachoweza kufanya au tunachowaomba.

(src)="12.8"> בסרט תיעודי על חייו של ג ׳ יהאד דיאב באורוגוואי , כתב העת אנפיביה טוען שהעסקה שהבטיחה את שחרורו היתה בעצם הסכם ״ בלתי רשמי ״ עם ארה ״ ב .
(trg)="10.7">Katika makala kuhusu maisha ya Jihad Diyab huko Uruguai, jarida la Anfibia linasema kuwa mpango uliosababisha kufunguliwa kwake ulikuwa ni makubaliano "yasiyo rasmi" na Marekani.

(src)="12.9"> במלים אחרות , אין שום מסמכים רשמיים המבססים את זכויותיהם של אסירים לשעבר .
(trg)="10.8">Kwa maneno mengine ni kuwa hakuna nyaraka rasmi zinazothibitisha haki za wafungwa hao wa zamani.

(src)="13.1"> הסרט התיעודי של אנפיביה בוחן גם את חייהם של אסירים ששוחררו מגואנטאנמו וחיים באירופה ובאפריקה , שם רבים מהם מתמודדים עם בעיות דומות .
(trg)="11.1">Jarida hilo la Anfibia pia lilichunguza maisha ya waliokuwa wafungwa wa Guantanamo ambao wengine wanaishi Ulaya na Afrika na kugundua kuwa wengi wanakutana na changamoto zinazofanana.

(src)="13.2"> אחד הגברים הללו , החי כעת בסלובניה , סיפר לכתב העת ״ זה לא חופש .
(trg)="11.2">Mmoja kati ya wanaume hao, kwa sasa anaishi nchini Slovakia aliliambia jarida kuwa “Huu sio uhuru.

(src)="13.3"> אנחנו עדיין אסירים .
(trg)="11.3">Bado tumefungwa.

(src)="13.4"> עזבתי את גואנטאנמו , אבל הוא בתוכי-כל הזמן .
(trg)="11.4">Nimeondoka Guantanamo lakini bado iko ndani yangu wakati wote.”

(src)="13.5"> ״ .
(trg)="11.5">Mfungwa mwingine ndani ya sinema aliyaita maisha yake baada ya kutoka gerezani "Guantanamo ya pili”

(src)="14.1"> מאז אפריל , כל האסירים המשוחררים באורוגוואי למעט דיאב חתמו על עסקה עם ארגון כבוד האדם הבינלאומי ( SEDHU בספרדית ) שתאפשר להם קבלת סיוע כלכלי .
(trg)="12.1">Tangu Aprili, wafungwa hao wote wa zamani walioko Uruguai isipokuwa Diyab walisaini mpango wa Huduma ya Kiekumeni kwa Utu (SEDHU huko Hispania)wa kuwapa msaada wa kifedha.

(src)="14.3"> דיאב טוען שהפציעה בגבו מונעת ממנו לעבוד , וכן שהסיוע הכלכלי שהוצע לו אינו מספק לכלכל אותו ובוודאי שלא את משפחתו .
(trg)="13.2">Diyab anasema kuwa majeraha ya mgongo wake yanamzuia kufanya kazi na akaongeza kusema kuwa msaada huo wa fedha hautoshelezi kuendesha maisha yake achilia mbali familia.

(src)="15.1"> דיאב הוא היחיד מששת האסירים שהגיע לגואנטאנמו כשהוא נשוי ואב לילדים .
(trg)="14.1">Diyab ndie mfungwa pekee kati ya sita walioingia Guantanamo akiwa na mke na watoto wake.

(src)="15.2"> הוא היחיד בקבוצה שאומר שהוא רוצה לעזוב את אורוגוואי ולעבור למדינה דוברת ערבית , על מנת להקים בית עם משפחתו .
(trg)="14.2">Katika kundi lake, ndiye pekee anayesema anataka kuondoka nchini Uruguay kwenda katika nchi ya Kiarabu anakotegemea kuishi na familia yake.

(src)="16.1"> אז לאן עכשיו ?
(trg)="14.3">Kwa hiyo, Ni wapi sasa?

(src)="17.1"> האתגר הבא העומד בפני דיאב הוא למצוא בית חדש .
(trg)="15.1">Changamoto inayomkabili Diyab kwa sasa ni kupata makazi mapya.

(src)="17.2"> בריאיון עם העלון העצמאי La Diaria , חבר הפרלמנט לוסיה טופולנסקי-שהיה כלוא בזמן השלטון הרודני באורוגוואי-הבטיח שהממשלה מחפשת לו פתרון .
(trg)="15.2">Ndani ya mahojiano aliyoyafanya na jarida huru liitwalo La Diaria, Senator Lucía Topolansky aliyefungwa enzi za serikali ya kidikteta ya Uruguai aliahidi kuwa serikali inaendelea kutafuta suluhu:

(src)="17.3"> מה שעלינו לעשות זה לחפש מדינה שתקבל אותו .
(trg)="15.3">Tunachotakiwa kufanya ni kutafuta nchi itakayo mkubali.

(src)="17.4"> וזו לא הבעיה רק של אורוגוואי או רק שלו-זוהי בעיה של העולם .
(trg)="15.4">Na hili sio tatizo la Uruguai au la kwake pekee, ni tatizo la dunia nzima.

(src)="17.5"> בספטמבר , ממשלת אורוגוואי פרסמה מזכר המאשר שהיא מחפשת מדינה המוכנה לקבל את דיאב ומשפחתו .
(trg)="15.5">Mwezi Septemba serikali ya Uruguai ilitoa tamko kuthibitisha kuwa inatafuta nchi ambayo iko tayari kumpokea Diyab na familia yake.

(src)="17.6"> פקידים אומרים שהם עושים כל שביכולתם ומבקשים בדיאב להפסיק את שביתת הרעב ו ״ לכבד את עיקרון החיים ״ .
(trg)="15.6">Maofisa wa serikali walisema kuwa wanafanya kila wawezalo kumuomba Diyab kusitisha mgomo wa kula ili "kuheshimu kanuni ya uhai."

(src)="18.1"> אך תהליכי המשא-ומתן הראו התקדמות איטית מאוד .
(trg)="16.1">Hata hivyo majadiliano hayo yameonesha mafanikio kidogo.

(src)="19.2"> כשנעצר בלאהור על ידי המשטרה הפקיסטנית בשנת 2002 , הוא התגורר בדירה שהוחזקה על ידי הטאליבן ומכר דבש כדי לפרנס את משפחתו .
(trg)="17.2">Alipokamatwa huko mjini Lahore na polisi wa Pakistani mwaka 2002, alikuwa akiishi katika nyumba iliyofanyiwa marekebisho na Taliban na alikuwa akiuza asali ili kujikimu yeye na familia yake.

(src)="20.1"> הקבצים קושרים בין דיאב לחברי אל-קאעידה , ומזהים אותו כגורם ״ סיכון גבוה ״ בעל ״ אינטליגנציה גבוהה ״ וכ ״ איום לארצות הברית ״ .
(trg)="18.1">Jalada lililomuhusisha Diyab na wafuasi wa al-Qaida, lilimtambulisha kama " mtu hatari" "intelijensia ya hali ya juu" na "tishio kwa Marekani.”

(src)="20.2"> הוא הואשם בזיוף מסמכים ודרכונים לאירגוני טרור .
(trg)="18.2">Alidaiwa kuhusika na kughushi nyaraka na hati za kusafiria kwa ajili ya jumuiya za kigaidi.

(src)="20.3"> למרות שהוחזק יותר מעשר שנים בבית מעצר אמריקאי , מעולם לא הוגש נגדו כתב תביעה .
(trg)="18.3">Akiwa kizuizini mwa Marekani kwa zaidi ya muongo mmoja, hakuwahi kufunguliwa mashtaka rasmi kwa kosa lolote.

(src)="20.4"> דיאב מכחיש את כל ההאשמות .
(trg)="18.4">Diyab alikana mashtaka yote.

(src)="21.2"> בינתיים , דיאב ממתין כפי שהמתין במשך 13 שנים בכלא .
(trg)="19.2">Ni wakati wa kurudia kufanya kile alichokifanya miaka 13 akiwa gerezani, Diyab anasubiri.

(src)="21.3"> בריאיון עם CNN , הוא הצהיר :
(trg)="19.3">Ndani ya mahojiano na shirika la habari la CNN,alisema kuwa:

(src)="21.5"> השבוע , לאחר 54 ימים של שביתת רעב , דיאב אובחן כסובל מתרדמת שטחית .
(trg)="19.5">Juma hili, baada ya siku 54 za kukataa kula, Diyab aligundulika kuwa na tatizo la "kupoteza fahamu juu juu."

(src)="21.6"> לפי העיתון La Diaria , הוא חתם בעבר על מסמך שדוחה התערבות רפואית ״ אפילו במצב של סכנת חיים ״ , אך הוא הסכים לאחר מכן לקבל האכלה תוך-ורידית .
(trg)="19.6">Kulingana na gazeti la La Diaria, hapo nyuma alisaini nyaraka akikataa kuingiliwa kati na huduma za kitabibu "hata kama maisha yake yatakuwa hatarini" lakini baadaye alikubali kulishwa kwa njia ya mishipa.

(src)="21.7"> הרופא שמסייע לדיאב אומר שמצב בריאותו כרגע הוא ״ קריטי ״ ושהוא ״ בסיכון גבוה למוות פתאומי ״ .
(trg)="19.7">Daktari anayemuhudumia Diyab anasema kuwa hali yake ya sasa ni "mbaya" inayoweza kusababisha "kifo cha ghafla".

(src)="21.8"> בנוסף להתדרדרות במצבו , המתווך בינו לבין ממשלת אורוגוואי התפטר מתפקידו .
(trg)="19.8">Pamoja na hali yake inayotetereka, msulihishi baina yake na serikali ya Uruguai ameiacha kesi yake.

(src)="22.1"> למרות הכל , שביתת הרעב ממשיכה בעוד דיאב ממתין לתשובה לבקשתו .
(trg)="20.1">Hata hivyo, mgomo wa kula utaendelea wakati Diyab anasubiria majibu ya ombi lake.

# he/2016_11_03_453_.xml.gz
# sw/2016_11_mazungumzo-ya-gv-hisia-zetu-siku-sita-kabla-ya-uchaguzi-wa-marekani_.xml.gz


(src)="1.1"> שיחת קולות גלובאליים : כיצד אנחנו מרגישים שישה ימים לפני הבחירות בארה ״ ב
(trg)="1.1">Mazungumzo ya GV: Hisia Zetu Siku Sita Kabla ya Uchaguzi wa Marekani

(src)="1.2"> מי ינצח בשמיני לנובמבר : טראמפ , הילארי , או שטיין ?
(trg)="1.2">Ni nani ataibuka mshindi siku ya Novemba 8: Trump, Hillary au Stein?

(src)="2.1"> למרות שרבים מהמחברים של קולות גלובאליים אינם יכולים להצביע בארה ״ ב , כולנו חשים מאוד מעורבים במירוץ לנשיאות האמריקאי הנוכחי .
(trg)="2.1">Hata kama waandishi wetu wengi wa Global Voices hawataweza kupiga kura nchini Marekani, tunajisikia kuguswa kwenye uchaguzi huu wa Urais kama ilivyokuwa kwenye chaguzi nyinginezo.

(src)="3.1"> השאלות שעולות בראשנו : האם ארה ״ ב תהיה יותר מעורבת או מבודדת מבחינה עולמית ?
(trg)="3.1">Maswali tunayojiuliza: Je, Marekani itakuwa na ushirikiano zaidi na mataifa mengine au itajitenga?

(src)="3.2"> האם נשיאה אישה בארה ״ ב תשנה את מצבן של נשים בעולם ?
(trg)="3.2">Rais mwanamke nchini Marekani ataweza kuleta auheni kwa mambo yanayowahusu wanawake kote duniani?

(src)="3.3"> האם יהיה יותר קשה למהגרים וקבוצות מיעוטים לחיות בארה ״ ב ?
(trg)="3.3">Itawawia vigumu kwa makundi ya wahamiaji na watu wa chini kuishi nchini Marekani?

(src)="6.1"> השיחה הזו מנוהלת על ידי נווין תומפסון , עורך תקשורת חברתית וקולות גלובאליים יפן .
(trg)="6.1">Majadiliano haya yalisimamiwa na Nevin Thompson, Mhariri wa mitandao ya Kijamii wa Global Voices na pia ni mhariri wa Japan.

(src)="7.1"> בשבוע שעבר , עורך התקשורת החברתית שלנו מביירות , זוהור מחמוד , ניהל את הדיון בין עורך קולות גלובאליים מזרח תיכון וצפון אפריקה , ג ׳ ואי איוב , טורי אגרמן , מצביעה אמריקאית ומחברת בנושא איראן הממוקמת באמסטרדם , וסהאר גאזי , עורכת ראשית בקולות גלובאליים ומצביעה אמריקאית הממוקמת בסאן פראנסיסקו .
(trg)="7.1">Wiki iliyopita, mhariri wetu wa mitandao ya kijamii kutoka Beirut-Zuhour Mahmoud alisimamia mjadala uliowahusisha mhariri wetu wa Mashariki ya kati na Afrika Kaskazini-Joey Ayoub, Tori Egherman aliyeko Amsterdam, mpiga kura wa Marekani na pia ni mchangiaji wa Global Voices kutoka Iran, pamoja na Sahar Ghazi, aliyeko San Francisco, mpiga kura katika uchaguzi wa Marekani na pia ni Mhariri Mtendaji wa Global Voices.

(src)="7.2"> אפשר לצפות בפרק משבוע שעבר כאן .
(trg)="7.2">Unaweza Kuitazama makala hiyo hapa.