# en/2008_08_17_angola-brazil-a-culture-shock-divide_.xml.gz
# sw/2008_08_angola-brazil-mshituko-na-utengano-wa-kitamaduni_.xml.gz


(src)="1.1"> Angola , Brazil : A culture shock divide · Global Voices
(trg)="1.1"> Angola , Brazil : Mshituko na Utengano wa Kitamaduni

(src)="2.1"> Polychromed woodcarving of an Orixá by Luiz Paulino da Cunha .
(trg)="2.1"> Kinyago cha mtumwa mweusi kilichochongwa na Luiz Paulino da Cunha .

(src)="2.2"> Photo by Children At Risk Foundation
(trg)="2.2"> Picha kwa hisani ya Asasi ya Watoto Walio Hatarini .

(src)="3.1"> Angola and Brazil have a special relationship towards each other , partially because of their common language and their shared colonial past - both countries were part of the Portuguese Empire - and the cultural ties that stem from this shared history .
(trg)="3.1"> Angola na Brazil zina uhusiano maalum baina yao , kutokana na matumizi ya lugha moja na pamoja na historia yao ya kutawaliwa huko nyuma - nchi hizi mbili zilikuwa sehemu ya himaya ya Wareno – na utamaduni wa pamoja unaotoka na historia ya asili moja .

(src)="3.2"> Since 2000 , commerce between the two countries has started to grow and it is now booming .
(trg)="3.2"> Tangu mwaka 2000 , biashara kati ya mataifa haya mawili ilianza kukuwa na sasa inachanua .

(src)="3.3"> According to the Association of Brazilian Companies in Angola ( AEBRAN ) , trade between the two countries has risen six-fold since 2002 .
(trg)="3.3"> Kwa mujibu wa Chama cha Makampuni ya KiBrazili nchini Angola ( AEBRAN ) , biashara kati ya mataifa mawili haya imekuwa kwa mara sita zaidi tangu mwaka 2002.

(src)="4.1"> With the increase in trade , the presence of Brazilian companies in Angola has also grown .
(trg)="4.1"> Kutokana na kuongezeka huko kwa biashara , uwepo wa makampuni ya Brazili nchini Angola pia kumeongezeka .

(src)="4.2"> Consequently , immigration from Brazil to Angola has increased too , 70 percent over the last five years .
(trg)="4.2"> Kumepelekea , pia ongezeko la uhamiaji kutoka Brazili kwenda Angola kwa kadri ya asilimia 70 kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita .

(src)="4.3"> There are an estimated 5,000 Brazilians registered in Angola , mainly working for construction , mining and agribusiness companies .
(trg)="4.3"> Inakadiriwa kuwa kuna Wabrazili 5,000 waliosajiliwa nchini Angola haswa wanaojishughulisha na masuala ya ujenzi , uchimbaji madini na biashara za mazao ya kilimo .

(src)="4.4"> This new development in Angolan history , a country which was more accustomed to immigration to the other side of the Atlantic , leads to an unavoidable culture shock for both Brazilians and Angolans alike .
(trg)="4.4"> Maendeleo haya mapya katika historia ya Angola , nchi iliyozoea kuwa na uhamiaji kuelekea ng'ambo nyingine ya Atlantiki , yanapelekea kwenye mtikisiko wa kiutamaduni usioweza kuepukika kwa wote , Wabrazili na Waangola pia .

(src)="5.1"> Below are two entire blog posts showing different perspectives of one people towards the other , raising issues of immigration , racism , ethnicity and mutual respect .
(trg)="5.1"> Hapa chini kuna habari zilizopachikwa katika kurasa za blogu mbili zikionyesha mitazamo tofauti baina ya watu wawili kwa kuibua masuala muhimu kama uhamiaji , ubaguzi wa rangi , ukabila na heshima miongoni mwa watu .

(src)="5.2"> Above all , they illustrate the complex and diverse relationship - with all of the inevitable similarities and differences - of siblings growing up an ocean apart .
(trg)="5.2"> Zaidi ya yote , wanabainisha mahusiano ya namna mbalimbali na yenye mchanganyiko - kwa kuwianisha yale yanayofanana na yanayotofautiana - miongoni mwa watoto hao waliotenganishwa na bahari wakati wa makuzi yao .

(src)="7.1"> Polychromed woodcarving of a slave by Luiz Paulino da Cunha .
(trg)="7.1"> Kinyago cha mtumwa mweusi kilichochongwa na Luiz Paulino da Cunha .

(src)="7.2"> Photo by Children At Risk Foundation
(trg)="7.2"> Picha kwa hisani ya Asasi ya Watoto Walio Hatarini .

(src)="8.1"> Migas , a Brazilian living in Luanda , says the following :
(trg)="8.1"> Migas , Mbrazili anayeishi Luanda , anasema yafuatayo :

(src)="9.1"> The Negro was uprooted from his land and sold as merchandise , enslaved .
(trg)="11.1"> Mtu mweusi aling'olewa kutoka katika ardhi yake na kuuzwa kama bidhaa , utumwani .

(src)="9.2"> In Brazil he arrived as slave , object ; from his land he departed as a free man .
(trg)="11.2"> Aliwasili nchini Brazili kama mtumwa , kifaa ; kutoka katika ardhi yake alitoka kama mtu huru .

(src)="9.3"> During the journey , the slave traffic , he lost his personality , but his culture , his history , his landscape , his experiences ; they came with him .
(trg)="11.3"> Wakati wa safari , safari ya utumwani , alipoteza utu wake , lakini utamaduni wake , historia yake , nchi yake , na uzoefu wake alikuja navyo .

(src)="10.1"> 300-year history of Negro enslavement in Brazil has made an impact on this country .
(trg)="12.1"> Miaka 300 ya historia ya utumwa wa mtu mweusi nchini Brazili imeacha athari kubwa ndani ya nchi hiyo .

(src)="10.2"> Candomblé is one such impact , a religion filled with many secrets , symbols and rituals known only to initiates but it is also a vital part of cultural expression in Brazil .
(trg)="12.2"> Candomblé ni mojawapo ya athari hizo , dini iliyojawa na siri nyingi , ishara za matambiko yanayofahamika tu kwa wanaopitipia matambiko hayo lakini pia ni ni sehemu muhimu ya utamaduni wa Brazili .

(src)="10.3"> There are no definitive numbers on how many people in Brazil follow Candomblé .
(trg)="12.3"> Hakuna idadi kamili kuhusiana na watu wangapi wanaabudu Candomblé .

(src)="10.4"> The government estimates , conservatively , that there are more than 300,000 centers of worship for Brazil 's Afro-Brazilian religions , which include Candomblé .
(trg)="12.4"> Serikali inakadiria , kihafidhina , kwamba kuna vituo zaidi ya 300,000 vya kuabudia imani za Wabrazili wenye asili ya Afrika , ambavyo vinajumuisha Candomblé .

(src)="10.5"> Those participating in these faiths are thought to make-up at least one-third of Brazil 's near 170 million inhabitants .
(trg)="12.5"> Wanaoshiriki katika imani hizo wanadhaniwa kufikia angalau theluthi moja ya watu wote wa Brazili wanaokaribia milioni 170.

(src)="10.6"> Many practice both Catholicism and Candomblé .
(trg)="12.6"> Wengi wanaabudu katika Ukatoliki na Candomblé .

(src)="11.1"> Bahia , the state with the largest percentage of Blacks , is the capital of this religion , which closely follows its African roots and traditions among the Yoruba people of Nigeria and the Bantu people of Angola and the Congo .
(trg)="12.7"> Bahia , jimbo ambalo lina asilimia kubwa zaidi ya watu weusi , ndiyo makao makuu ya dini hii , ambayo inafuata kwa karibu asili yake ya Kiafrika na hasa tamaduni za Kiyoruba za Nigeria na za Kibantu za Angola na Kongo .

(src)="11.2"> Yoruban traditions , including the most commonly used names of the Orixás ( gods of the African pantheon ) , predominate .
(trg)="12.8"> Tamaduni za Kiyoruba zinazojumuisha majina yanayotumika sana ya Orisha ( miungu ya mahekalu ya Kiafrika ) , bado inatawala sana .

(src)="12.1"> Today Candomblé is officially recognized and protected by the government of Brazil .
(trg)="12.9"> Hivi sasa Candomblé inatambulika rasmi na inalindwa na serikali ya Brazil .

(src)="12.2"> However , during the period of slavery and for many decades following its abolition in Brazil in 1888 , Candomblé practices were banned by the government and by the Catholic church , and its practitioners were severely punished .
(trg)="12.10"> Hata hivyo , enzi za utumwa na miongo mingine iliyofuata baada ya kukomeshwa kwa biashara hiyo ya watu nchini Brazil mwaka 1888 , ibada za Candomblé zilipigwa marufuku na serikali na kanisa Katoliki , na wafuasi wake waliadhibiwa vikali .

# en/2008_08_08_angola-countdown-to-the-long-awaited-elections_.xml.gz
# sw/2008_08_angola-kuelekea-uchaguzi-unaosubiriwa-kwa-muda-mrefu_.xml.gz


(src)="1.1"> Angola : Countdown to the long awaited elections · Global Voices
(trg)="1.1"> Angola : Kuelekea Uchaguzi Unaosubiriwa Kwa Muda Mrefu

(src)="1.2"> It is less than a month for Angola to experience one of the most anticipated episodes in its history .
(trg)="1.2"> Ni chini ya chini ya mwezi mmoja kwa Angola kabla ya kuingia zoezi linalosubiriwa zaidi katika aya za historia yake .

(src)="1.3"> Sixteen years since the last elections , Angolans will once again have the opportunity to exercise their right to vote in the upcoming legislative elections , taking place from 5 through 6 September .
(trg)="1.3"> Miaka kumi na sita baada ya uchaguzi wake wa mwisho , Waangola kwa mara nyingine tena watapata fursa ya kutumia haki yao ya kupiga kura katika uchaguzi wa bunge , utakaofanyika kuanzia tarehe 5 mpaka 9 Septemba .

(src)="2.1"> The atmosphere is quiet , although there are different feelings among the population .
(trg)="2.1"> Hali ni ya ukimya , japokuwa kuna hisia zinazotofautiana katika umma .

(src)="2.2"> The more affluent people say they are going abroad ; some smile and guarantee that nothing will happen because Angolans don 't want war and suffering anymore ; while others rush to stores to buy staple goods , just in case the devil pays and things go wrong , as happened in 1992 .
(trg)="2.2"> Watu wanojiweza wanasema watakwenda ughaibuni ; wengine wanatabasamu na kujihakikishia kwamba hakuna litakalotokea kwani Waangola hawataki tena vita na mateso ; wakati wengine wanakimbilia madukani kunua vyakula , ikiwa muovu atalipa na mambo yataenda vibaya , kama ilivyotokea mwaka 1992.

(src)="2.3"> As a reminder , at that time the largest opposition party , UNITA , contested the polls and fighting broke out , leading to a resumption of the civil war that ended ten years later , with the death of the charismatic leader of that party , Jonas Savimbi .
(trg)="2.3"> Kama itakumbukwa , wakati ule chama kikubwa cha upinzani , UNITA , kilishindana katika uchaguzi na mapigano yalizuka , yakapelekea kuibuka tena kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilimalizika miaka kumi baadaye , na kifo cha kiongozi mwenye mvuto mkubwa wa chama hicho , Jonas Savimbi .

(src)="3.1"> When it comes to foreign businessmen based in Angola , they have no intention of returning to their home countries .
(trg)="4.6"> Kiongozi huyo aliongeza kwamba ni muhimu " kuheshimu mitazamo na fikra za wengine " bila kutumia " maneno au vitendo vya vurugu " .

(src)="3.2"> The business community is confident that everything will remain the same after the elections and that it is not necessary to change professional commitments .
(trg)="5.1"> Tunategemea kuwa wapiga kura milioni 8.3 watakuwa na mazingira yenye amani kwa upigaji kura na watafanya hivyo katika njia ya safi na inayoeleweka vyema .

(src)="3.3"> Jotacê Carranca makes the following reflection on the local atmosphere :
(trg)="5.2"> Kuna zaidi ya vituo 12 elfu vya kupigia kura katika dola ya kitaifa .

# en/2008_08_06_arabeyes-mauritanian-president-ousted-in-military-coup-detat_.xml.gz
# sw/2008_08_arabeyes-rais-wa-mauritania-aliyepinduliwa-katika-mapinduzi-ya-kijeshi_.xml.gz


(src)="1.1"> Arabeyes : Mauritanian President Ousted in Military Coup d 'état · Global Voices
(trg)="1.1"> Arabeyes : Rais wa Mauritania Aliyepinduliwa Katika mapinduzi ya Kijeshi

(src)="1.2"> Army commanders ousted Mauritania 's first freely elected president in two decades , President Sidi Ould Cheikh Abdallahi , in a military coup d 'état Wednesday after political feuding over the firing of the country 's four top generals .
(trg)="2.1"> MAKAMANDA wa jeshi wamemuondoa madarakani Rais Sidi Ould Cheikh Abdallahi , rais wa kwanza kuchaguliwa katika uchaguzi huru katika miongo miwili , katika mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa Jumatano iliyopita baada ya mtafaruku wa kisiasa uliotokana na rais huyo kuwatimua kazi majenerali wanne wa ngazi za juu wa jeshi .

(src)="1.3"> Military commanders announced the formation of a new state council and its leader , General Mohamed Ould Abdel Aziz ( one of the four fired generals ) , on state radio and television stations .
(trg)="2.2"> Makamanda wa jeshi walitangaza kuundwa kwa Baraza jipya la taifa na kiongozi wake , Jenerali Mohamed Ould Abdel Aziz ( mmoja kati ya majenerali wanne wa jeshi waliotimuliwa ) , kwenye radio na vituo vya televisheni vya serikali .

(src)="1.4"> General Abdel Aziz was also involved in a 2005 coup d 'état in Mauritania .
(trg)="2.3"> Jenerali Abdel Aziz ni miongoni mwa walioshiriki mapinduzi ya kijeshi nchini Mauritania mwaka 2005.

(src)="2.1"> Algerian The Moor Next Door has been blogging the story intensively and reports :
(trg)="3.1"> Bloga kutoka Algeria The Moor next Door amekuwa akiblogu habari hii kwa kina anaripoti :

(src)="2.2"> Talking to informed Mauritanians , some of them saw the coup coming during the summer ( as it did ) , in the autumn , or not at all .
(trg)="3.3"> Hisia zangu mara zote zilikuwa zikinielekeza kwamba mapinduzi haya yangefanyika majira ya kiangazi ( Sijawahi kuandika bayana juu ya hili , lakini nimelielezea hili katika majadiliano na sikutaka kuchangia lolote kuhusiana na sakata hili .

(src)="2.3"> My sense was always that the coup would come this summer ( I never wrote this expressly but I expressed this view in discussion and refrained from commenting on the crisis ( 1 ) because Western Sahara Info. covered it well and there is not point in competing when you ’ re one of two or three bloggers paying attention to it , ( 2 ) I wanted to make sure that if I “ predicted ” it I would not be wrong ; I could have said , “ by the end of May / June / July / August Sidi s government ’ will be no more and been ” wrong ; I ’ m no weather man , and ( 3 ) I ’ ve yet to encounter a Mauritanian that had positive things to say about Sidi beyond his golden personality ) .
(trg)="3.4"> ( 1 ) kwa sababu Western Sahara Info . taarifa za kutoka Sahara Magharibi zilielezea kinaganaga na hakukuwa na haja ya kushindana ikiwa wewe ni mmoja wa mabloga wawili au watatu unakuwa miongonimwa wanaofuatilia sakata hili kwa karibu sana .
(trg)="3.5"> ( 2 ) nilitaka kuhakikisha kwamba kama 'ningetabiri ' jambo hili nisingekosea ; Ningeweza kutabiri kuwa 'Mwishoni mwa miezi ya Mei , Juni , Julai na Agosti Serikali ya Rais Sidi , isingelikuwapo tena ' na ningekuwa nimekosea ; mimi si mtabiri wa hali ya hewa , na ( 3 ) sijawahi kukutana na raia wa Mmauritania ambaye lolote jema la kumzungumza kuhusu Sidi , ukiachilia mbali uzuri wa wajihi wake . )

(src)="2.4"> One of the major pressures that forced Sidi to act the way he did towards the end was the threat of a commission being formed to investigate the financial side of his wife ’ s foundation , which would surely have done him in ever more deeply .
(trg)="3.6"> Mojawapo ya mashinikizo yaliyomfanya Rais Sidi afanye alivyofanya ni kuwapo tishio la kuundwa tume huru ya kuchunguza mapesa ya mfuko wa maendeleo wa mkewe , tume ambayo ingemuweka hata yeye mwenyewe pabaya zaidi .

(src)="2.5"> The commission might even have made his administration s ridiculous personal expenditures ’ public .
(trg)="3.7"> Tume hiyo pia ingeufanya utawala wa Rais Sidi kituko kutokana na matumizi mabaya ya fedha za umma .

(src)="2.6"> For instance , I am told that his air travels alone cost the state some $ 2 billion , on chartered jets , his family , full entourage , and various other luxuries .
(trg)="3.8"> Kwa mfano , nimeambiwa kuwa , safari zake za ndege za nje ziliigharimu serikali zaidi ya dola za Marekani mbili bilioni , kwa kukodisha ndege za kifahari yeye na familia yake na ujumbe wake pamoja na anasa zingine zisizokuwa za lazima .

(src)="2.7"> He was between a rock and a hard place : Either he would be forced to step down ( a la Olmert ) in total shame , or he would be impelled to dissolve parliament and reorganize his government , which would precipitate a coup such as today s ’ , allowing him to save political face .
(trg)="3.9"> Kwa hakika alikuwa katika wakati mgumu : Ama angelazimika kujiuzulu ( kwa mujibu wa Olmert ) katika aibu kubwa au angelazimika kuvunja bunge na hivyo kuunda serikali yake upya , hali ambayo ingempeleka katika mapinduzi kama haya tuliyoyoyashuhudia , ambayo angalau imeficha aibu yake kisiasa .

(src)="2.8"> Flanked on both sides , he moved in desperation and met his fate .
(trg)="3.10"> Alibanwa pande zote na alikuwa hana pa kutokea zaidi ya kukumbana na hatima yake .

(src)="2.9"> Western Sahara Info has been blogging the crisis from its outset , and today provided up-to-the-minute information on the coup , including a brief analysis :
(trg)="3.11"> Western Sahara Info amekuwa akiblogu mgogoro huu tokea ulipoanza , na leo ametuletea habari za mapinduzi hayo ya kijeshi kama zinavyotokea dakika kwa dakika , pamoja na muhtasari wa unyambuzi :

(src)="2.10"> Quick analysis , which I may regret : a tragedy for Mauritanian democracy , on the one hand , but that didn 't stand much of a chance anyway ; but more importantly , a giant setback for the country 's broader chances of political development .
(trg)="3.12"> Uchambuzi wa harakaharaka , ambao naweza kuujutia : balaa kwa demokrasia ya Mauritania , kwa upande mmoja , ( demokrasia ) ambayo haikuwa na nafasi , lakini muhimu zaidi ni kuwa ( mapinduzi haya ) yamerudisha nyuma nafasi iliyokuwepo kwa maendeleo ya kisiasa .

(src)="2.11"> While President Abdellahi and his cronies aren 't exactly angels , Generals Ghazouani and Abdelaziz represent the very worst military-parasitic element of the Mauritanian regime , and their refusal to let the civilian side of the regime settle down in power threatens to undo it completely in the long run .
(trg)="3.13"> Ingawa , Rais Abdellahi na washirika wake si malaika , lakini Majenerali Ghazouani na Abdelaziz wanawakilisha kundi baya la kinyonyaji katika utawala wa Mauritania , kwa kukataa kuruhusu utawala wa kiraia kutulia madarakani kwa kuwatishia kung'oa kabisa utawala wa kiraia hatimaye .

(src)="2.12"> If the last coup , in August 2005 , could be met with cautious understanding by the international community , having unseated President ould Tayaa , and eventually with praise as it led to a real transformation , this time around it is different .
(trg)="3.14"> Kama mapinduzi ya mwisho ya kijeshi yaliyotokea Agosti 2005 , yangalieleweka na Jumuiya ya Kimataifa baada ya kung'olewa kwa Rais Ould Tayaa , na hatimaye kupelekea mabadiliko makubwa , mapinduzi haya ya juzi yalikuwa tofauti saana .

(src)="2.13"> What happened in 2005 was that a military-personal-tribal dictatorship was overthrown and the chance arrived to replace it with a civilian semi-authoritarian structure that respected most democratic norms most of the time , and which made sensible moves towards national reconciliation , refugee return and economic development ; not heaven , but infinitely better .
(trg)="3.15"> Kilichotokea mwaka 2005 ilikuwa kwamba madikteta wa kijeshi walioegemea katika ukabila waling'atuliwa na nafasi ilijitokeza ikasimika badala yake utawala wa kiraia uliokuwa na muundo wa nusu-mabavu ambao uliruhusu desturi nyingi za kidemokrasia kwa muda mwingi zaidi , ( utawala huo ) ulishughulikia zaidi muwafaka wa kitaifa , urejeshwaji wa wakimbizi na maendeleo ya kiuchumi ; ingawa siyo hema , lakini ilikuwa bora .

(src)="2.14"> This change is now being reversed .
(trg)="3.16"> Mabadiliko haya hivi sasa yanageuzwa .

(src)="2.15"> The putschists — even though they are some of the same people as acted in 2005 — must be condemned and the result of the coup overturned if possible ; Mauritania had a golden opportunity to break its vicious circle , and it is now slipping away .
(trg)="3.17"> Wapinduaji - japokuwa wengine ni miongoni mwa wale waliofanya mwaka 2005 - - ni lazima walaumiwe na matokeo ya mapinduzi yabatilishwe kama inawezekana ; Mauritania ilikuwa na fursa ya pekee kuweza kuvunja mzunguko huu usiokwisha , na sasa ( fursa hiyo ya pekee ) inaponyoka .

(src)="2.16"> Roads to Iraq , in a post entitled " American orchestrated coup in Mauritania , " reports the news as well :
(trg)="3.18"> Blogu ya Roads To Iraq , katikaujumbe wenye kichwa cha habari " Wamarekani walipanga mapinduzi nchini Mauritania , " inaripoti habari hiyo vile vile :

(src)="2.17"> Things are happening rapidly in Mauritania , started with a coup this morning , issuing the statement “ no 1 ” on the Mauritanian TV , changing the Head of the TV because he refused to cooperate with the army chief who staged the coup , and announcing a new military junta .
(trg)="4.1"> Mambo yanabadilika kwa kasi sana nchini Mauritania , imeanza na mapinduzi asubuhi hii , kwa kutoa " taarifa nambari moja " katika kituo cha televisheni cha Mauritania , Mkuu wa kituo hicho cha televisheni
(trg)="5.1"> alibadilishwa sababu alikataa kushirikiana na mkuu wa jeshi aliyeandaa mapinduzi na kumtangaza mtawala mpya wa kijeshi .

(src)="2.18"> In Egypt , Bella says what happened in Mauritania proved that Arabs weren 't cut for democracy .
(trg)="5.2"> Huko Misri , Bella anasema kilichotokea Mauritania kimedhihirisha kuwa Waarabu hawakupangwa kwa demokrasia .

(src)="3.1"> It seems that democracy wasn 't made for people like us - who cannot breathe outside military rule .
(trg)="5.3"> Inaonekana demokrasia haikuumbwa kwa watu kama sisi - ambao hatuwezi kupumua nje ya tawala za kijeshi .

(src)="4.1"> After giving us a brief history of Mauritania 's young democracy , Bella writes :
(trg)="5.4"> Baada ya kutupa historia fupi ya demokrasia changa ya Mauritania Bella anaandika :

(src)="5.1"> This way , Mauritania , which was just about to reap the fruit of democracy in a pioneering move which the entire region was eyeing with excitement , things return to what they were originally , and the military intervened and the coup happened .
(trg)="5.5"> Kwa njia hii , Mauritania , ambayo ilikuwa ianze kuvuna matunda ya demokrasia katika msukumo wa kiasisi ambao eneo lote la mataifa ya jirani yalikuwa yanaungalia kwa shauku , mambo yamerejea kule yalikotoka kiasili , na wanajeshi wakaingilia kati na mapinduzi kutokea .

(src)="6.1"> Kuwaiti Wild Il Deera poses a few questions about the coup .
(trg)="5.6"> Bloga wa Kuwaiti Wild Il Deera anahoji maswali machache kuhusiana na mapinduzi haya .

(src)="7.1"> ألم يكن الرئيس الموريتاني رئيساً منتخباً من الشعب ؟
(trg)="5.7"> Anauliza :

(src)="9.1"> What is the stance of the Arab League from the leaders of this coup ?
(trg)="6.1"> Jumuiya ya Kiarabu ina msimamo gani kuhusu viongozi wa mapinduzi haya ?

(src)="10.1"> Wasn 't the Mauritanian leader elected by his people ?
(trg)="7.1"> Hivi huyu kiongozi wa Mauritania hakuchaguliwa na watu wake ?

(src)="11.1"> How can a political group , like the Arab League , which demands that it is respected in Arab and international arenas allow such a military coup to take place in one of its member countries ?
(trg)="8.1"> Hivi inawezekanaje kundi la kisiasa , kama Jumuiya ya Kiarabu , ambayo inataka kuheshimiwa katika jamii ya Kiarabu na katika ulingo wa kimataifa ikaruhusu mapinduzi kama haya kufanyika katika moja ya mataifa wanachama wake ?

(src)="12.1"> Prolific Moroccan blogger Larbi linked to a news article , remarking :
(trg)="8.7"> Mwishoni KABOBfest , ambaye huwa anaingiza vichekesho katika kila hali , anatoa maoni yenye mzaha :

(src)="12.2"> Whereas coup culture in a lot of countries is a thing of the past ( e.g. , Syria ain 't had a coup in a few decades ) some countries like to kick it old skool , harking back to when it seemed like there was a coup-a-week somewhere in the world .
(trg)="8.8"> Wakati utamaduni wa mapinduzi katika mataifa mengi ni utamaduni uliopitwa na wakati ( kama vile Syria hakujapata kutokea mapinduzi kwa miongo kadhaa sasa ) Baadhi ya mataifa yanapendelea mitindo ya kizamani , rejea pale ambapo ianonekana palikuwa na mapinduzi kama juma moja lililopita sehemu fulani hapa duniani .

(src)="12.3"> While Mauritania isn 't Fiji , they are keeping the tradition of pointless coups alive and well in the Arab world .
(trg)="8.9"> Wakati Mauritania siyo Fiji , wanadumisha utamaduni usio na maana wa mapinduzi katika dunia ya Waarabu .

(src)="12.4"> The Arabdemocracy blog also has an excellent " obituary " for the young democracy that was .
(trg)="8.10"> Blogu ya Arabdemocracy pia anayo taarifa ya maombolezo ya iliyokuwa demokrasia changa .

(src)="13.1"> Photo above is of Sidi Mohamed Ould Cheikh Abdallahi , by Marcello Casal Jr . / Abr ( Setember 2007 )
(trg)="9.1"> Picha ya hapo juu ni ya Sidi Mohamed Ould Cheikh Abdallahi iliyopigwa na Marcello Casal Jr./ Abr ( Septemba 2007 )

# en/2008_07_29_bangladesh-tweeting-and-blogging-an-earthqauke_.xml.gz
# sw/2008_08_bangladeshi-ku-twita-na-kublogu-tetemeko-la-ardhi_.xml.gz


(src)="1.1"> Bangladesh : Tweeting and blogging an earthquake · Global Voices
(trg)="1.1"> Bangladeshi : Ku-twita na kublogu tetemeko la ardhi

(src)="1.2"> A moderate earthquake jolted Dhaka city on the 27th of July approximately at 00 : 51 hours Bangladesh Time ( + 6 GMT ) .
(trg)="1.2"> Tetemeko la ardhi la wastani lilitikisa jiji la Dhaka siku ya tarehe 27 Julai mnamo muda wa saa 00:51 kwa saa za Bangladeshi ( +6 GMT ) .

(src)="1.3"> Russell John reports in his blog :
(trg)="1.3"> Russell John anaripoti katika blogu yake :

(src)="2.1"> I was lying on my bed talking to a friend on the phone , and I suddenly felt that the bed was shaking .
(trg)="2.1"> Nilikuwa nimelala kwenye kitanda changu huku nikongea kwa simu na rafiki yangu , na ghafla nikahisi kitanda kikitetemeka .

(src)="2.2"> Within 3 seconds , it stopped .
(trg)="2.2"> Ndani ya sekunde 3 kikasimama .

(src)="2.3"> My first impression was that a cat got under my bed and it was shaking it , but then I realised that it 's impossible as the bed is way too heavy .
(src)="2.4"> ( Plus there was no cat , I checked ! )
(trg)="2.3"> Kwa mtazamo wangu wa kwanza nilidhani ni paka aliyeingia kwenye uvungu wa kitanda na alikuwa akikisukuma-sukuma kitanda , lakini nikagundua kuwa hilo lisingewezekana kwani kitanda ni kizito mno . ( aidha hapakuwa na paka , nilihakikisha ! )

(src)="3.1"> I quickly asked my friends on IRC , and they said they felt it too .
(trg)="3.1"> Niliwauliza marafiki zangu haraka kwa kutumia IRC , na wao wakasema walihisi ( tetemeko ) pia .

(src)="3.2"> So it was an earthquake for real !
(trg)="4.1"> Kwa hiyo lilikuwa ni tetemeko kwa hakika !

(src)="3.3"> Quake in Dhaka at 12 : 51 AM !
(trg)="4.2"> Tetemeko ndani ya Dhaka saa 6.51 za usiku .

(src)="3.4"> Russell tweeted instantaneously :
(trg)="4.3"> Russell alituma ujumbe wa tweeter mara moja :

(src)="3.5"> Oh my God , I just felt an earthquake !
(trg)="4.4"> Mungu wangu , nimelihisi tetemeko la ardhi !

(src)="3.6"> Within next minutes , tweets started to appear confirming that they also felt the earthquake .
(trg)="4.5"> Katika dakika chache zilizofuata , jumbe za tweeter zikaanza kutokea zikithibitisha kwamba nao pia walilihisi tetetmeko .

(src)="4.1"> Munaz of Nothing to Lose and Nothing to Gain shared the tweeter feeds of some of his friends :
(trg)="5.1"> Munaz wa Nothing to lose and Nothing to Gain akaanza kuonyesha jumbe nyingine za tweeter zilizotumwa na marafiki zake :

(src)="6.1"> Information online was hard to come by ( except some Bangla blogs ) and everybody was trying to get updates .
(trg)="7.1"> Ilikuwa ni vigumu kupata habari katika mtandao ( isipokuwa kwenye blogu za lugha ya ki-bangla ) na kila mtu alikuwa akijaribu kupata habari zilizosasishwa .

(src)="6.2"> So Bauani of Information blog contacted U.S. Geological Survey , National Earthquake Information Center and posted the find :
(trg)="7.2"> Hivyo Bauani wa Information blogs akawasiliana na U.S geological Survey , National Earthquake Information na akabadika ujumbe wa alichokipata :

(src)="7.1"> Magnitude : 4.9
(trg)="8.1"> Ukubwa : 4.9

(src)="8.1"> Date-Time : Saturday , July 26 , 2008 at 18 : 51 : 49 UTC
(trg)="9.1"> Tarehe-saa : Jumamosi , Julai 26 , 2008 saa 18:51:49 UTC

(src)="9.1"> Location : 24.773 ° N , 90.480 ° E
(trg)="10.1"> Sehemu : 24.773°Maskasini , 90.480°Mashariki

(src)="10.1"> Depth : 5.2 km ( 3.2 miles ) ( poorly constrained )
(trg)="11.1"> Urefu kwa kwenda chini : km5.2 ( maili 3.2 )

(src)="11.1"> Region : BANGLADESH
(trg)="12.1"> Eneo : BANGLADESHI

(src)="12.1"> He was also posting the updates as and when available .
(trg)="12.2"> Alikuwa pia akituma jumbe zilizosasishwa kama na wakati habari mpya zilivyopatikana .

(src)="13.1"> Apparently no casualties were reported but it rattled the affected people of Dhaka , a populous mega city .
(trg)="13.1"> Hapakuwa na majeruhi walioripotiwa lakini ( tetemeko ) lilitikisa na kuwaathiri watu wa jiji kubwa lenye wakazi wengi la Dhaka .

(src)="14.1"> Rumi of In The Middle of Nowhere writes :
(trg)="14.1"> Rumi wa In the Middle of Nowhere anaandika :

(src)="16.1"> Map of all the major and minor tectonic plates of the world
(src)="17.1"> If you can locate Bangladesh in the world map , you will see two plate boundaries , i.e. two fault lines cross Bangladesh .... many scientists have been warning about the probability of a devastating 8-9 Richter scale catastrophic earthquake in the northeastern and southeastern parts of Bangladesh .
(trg)="16.1"> Kama naweza kuiona Bangladeshi kwenye ramani ya dunia , utaona mipaka ya sahani mbili , yaani , mistari ya inayokutanisha ( au kutenganisha ) magamba ya miamba-nchi inapita katikati ya Bangladeshi… wanasayansi wengi wamekuwa wakionya kuhusu uwezekano wa kutokea kwa tetemeko la ardhi lenye athari kubwa , 8-9 kwa vipimo vya skeli ya rikta huko kaskazini-mashariki na kusini-mashariki mwa Bangladeshi .

(src)="17.2"> So , ( a ) major earthquake is also possible in Bangladesh .
(trg)="16.2"> Kwa hiyo ( a ) kuna uwezekano wa kutokea tetemeko kubwa la ardhi katika Bangladeshi .

(src)="17.3"> Are we ready ?
(trg)="16.3"> Je tupo tayari ?

# en/2008_08_17_caribbean-lightning-bolt-strikes-beijing_.xml.gz
# sw/2008_08_karibeani-radi-ya-bolt-yaipiga-beijing_.xml.gz


(src)="1.1"> Caribbean : Lightning Bolt Strikes Beijing · Global Voices
(trg)="1.1"> Karibeani : Radi ya Bolt Yaipiga Beijing

(src)="2.1"> " Lightning Bolt " - Screenshot by hybridvigour .
(trg)="2.1">“ Radi ya Bolt” - Picha na hybridvigour .